Na Shomari Binda-Rorya
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi (CCM)mkoa wa Mara Julius Masubo maarufu ” Mfalme” amesema miaka 48 ya CCM ina maana kubwa kwa kuwa yapo maendeleo ambayo yamefikiwa.
Akizungumza kwenye sherehe za chama hicho zilizofanyika kimkoa Kijiji cha Kinesi wilayani Rorya amesema yapo maendeleo makubwa ambayo yanaonekana yaliyofanywa kuanzia serikali ya awamu ya kwanza.
Amesema kuanzia sekta ya elimu shule zimejengwa na kuboreshwa kwa madarasa na kupelekea watoto kupata elimu sehemu sahihi huku kwa sasa suala la kulipa ada ikiwa historia.
Masubo amesema sio tu kwenye elimu miradi ya maji imetekelezwa kila mahala na wanawake wametuliwa ndoo kichwani na kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
Mwenyekiti huyo wa Wazazi aliyemuwakilisha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara na Kamati ya Siasa amesema kuna kila sababu ya kusherehekea miaka hiyo na mazuri yaliyofanyika
” Tunaposherehekea miaka 48 ya CCM yapo mambo mengi mazuri ya kujivunia ambayo yamefanywa na chama chetu mkoa wa Mara na nchi nzima.
” Tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele tukijivunia hayo yaliyofanyika na tuendelee kuiamini CCM na kumchagua tena kwa miaka 5 Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan”,amesema.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo ametoa siku 7 kuhakikisha wananchi wa Kijiji hicho wanarudishiwa huduma ya maji baada ya kukosekana kwa miezi 8 kutokana na kuharibika kwa pampu.
Akizungumza kwenye sherehe hizo mbunge wa jimbo la Rorya Jafar Chege ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwapa fedha nyingi kwaajili ya miradi ya maendeleo.
Mjumbe wa Mamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara Nyihita Wilfred amesema upendo ni jambo la muhimu na kudai palipo na upendo hakuna kutofaitiana