Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) ameitaka Bodi ya Usimamizi na Stakabadhi za Ghala kuusimamia Mfumo wa Matumizi ya Kamera za Kidigital na Stika za Utambuzi wa Ghala ili wanunuzi wa ndani na nje ya nchi waweze kuuamini na kuutumia.
Vilevile, Dkt. Jafo ametoa rai kwa Wamiliki wa Maghala kutumia mfumo huo pamoja na stika zinatoa taarifa sahihi kuhusu ghala husika ili kuongeza uaminifu, uwazi kwa wanunuzi wa ndani na nje ya nchi pamoja na kuimarisha udhibiti na usalma wa mazao yanayohifadhiwa ghalani.
Dkt. Jafo ameyasema hayo Januari 31, 2025, Jijini Dodoma wakati akizundua Mfumo wa Matumizi ya Kamera za Kidigital na Stika za Utambuzi wa Ghala pamoja na kuongea na Watumishi wa Bodi hiyo.
Vilevile, Waziri Jafo ameanisha mafanikio yaliyopatikana kupitia Mfumo wa Stakabadhi ghalani ambao umechangia kuingezeka kwa bei ya mazao kama mbaazi na ufuta na kuwezesha kupatikan takribani Sh. Trilioni 1.4 kwenda kwa wakulima wanaotumia mfumo huo.
Kwa upande wa Watumishi wa Bodi hiyo Dkt.Jafo amewataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, uadilifu kwa kushirikiana na kupendana huku wakizingatia kutumia muda vizuri katika ili kuhakikisha Bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi, kuwanufaisha wakulima na kuongeza Pato la Taifa .
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Mkoanhuo uko tayari kuanza kutumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala wenye manufaa kwa wakulima na Taifa kwa ujumla mazao na bidhaa kama mazao, madini, mifugo n
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, Bw. Asangye Bangu, amesema kazi kubwa ya Bodi hiyo inayotoa huduma katika
Mikoa yote ni kuwezesha uhifadhi wa mazao, kuongeza ubora wa mazao hayo kutoa leseni za maghala, kurasmisha masoko pamoja na kuwezesha wakulima kupata bei nzuri ya mazao yao