Na Shomari Binda-Musoma
MWENYEKITI wa Mara Press Club Jacob Mugini amezindua semina za uwekezaji mkubwa wa kibiashara mkoani Mara huku watanzania wakitakiwa kujiunga na masoko ya hisa katika kujiinua kiuchumi.
Akizindua semina hizo kwa Waandishi wa Habari ambazo zitafanyika nchi nzima kupitia kampuni ya umma ya HAIPPA PLC Tanzania Limited amesema zipo faida kubwa kwenye uwekezaji.
Amesema kupitia wazo la HAIPPA PLC kuwafikia watanzania kuwapa elimu kuhusu uwekezaji hasa kwenye eneo la hisa linakuja kuwakomboa kiuchumi.
Mugini amesema kutokana na mawazo makubwa ya HAIPPA Waandishi wa Habari mkoani Mara watatoa ushirikiano kuhahakikisha elimu hiyo inawafikia wananchi na kufikia malengo
Awali akiwaseminisha Waandishi wa Habari mkoani Mara kwenye ukumbi wa Mwenbeni complex mkurugenzi wa kampuni ya umma ya HAIPPA PLC Tanzania Limited Boniphace Ndengo amesema ipo faida kubwa katika uwekezaji.
Amesema ili kutambua faida ya uwekezaji ndio iliyopelekea ofisi ya masuala ya uwekezaji kuwa chini ya ofisi ya Rais ili kuhudumia kwa karibu eneo hilo.
Ndengo amesema wananchi wanapaswa kununua hisa kupitia kampuni mbalimbali ili kuweza kujiinua kiuchumi
Akiilezea kampuni ya umma ya HAIPPA PLC Tanzania Limited amesema ina malengo makubwa ya kuwafikia wananchi kwa kutoa elimu hususani ya kujiunga na masoko ya hisa.
Amesema Waandishi wa Habari wanapaswa kutumia taaluma yao kwa kuwafikishia watanzania juu ya masoko ya hisa kwa kuwa tabia za hisa ni kupanda na zinainua haraka kiuchumi.
Mkurugenzi huyo wa HAIPPA PLC Tanzania Limited amesema wanayo malengo makubwa ya kuwa academy ya uwekezaji mkubwa barani Afrika katika kujiinua kiuchumi
” Tumeanzia semina zetu mkoani Mara masuala ya uwekezaji mkubwa na tumekusudia kufikisha elimu hii nchi nzima.
” Matajili wakubwa wote duniani wametajilika kupitia uwekezazaji kwenye masoko mbalimbali ya hisa hivyo tumekusudia kila mahala kuundwa makapuni ya umma ya uwekezaji kupitia HAIPPA”,amesema.