Home Kitaifa UJENZI WA UKUMBI WA MIKUTANO CCM MARA WAFIKIA ASILIMIA 65

UJENZI WA UKUMBI WA MIKUTANO CCM MARA WAFIKIA ASILIMIA 65

Na Shomari Binda – Musoma

Uwekezaji wa ujenzi wa ukumbi mkubwa wa mikutano unaojengwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara umefikia asilimia 65.

Hayo yamesemwa na Katibu wa chama hicho mkoa wa Mara, Ibrahim Mjanakher, alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Mzawa Blog jana, Januari 27, ofisini kwake.

Amesema kuwa hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo ni matokeo ya juhudi za wanachama na wadau mbalimbali wa chama hicho, kutoka ndani na nje ya mkoa wa Mara.

Mjanakher amesema kuwa hadi sasa, zaidi ya shilingi milioni 700 zimetumika katika ujenzi huo unaotarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 2,000 kwa wakati mmoja.

Amesema kuwa uwekezaji wa ukumbi huo ni sehemu ya maelekezo ya chama ngazi ya taifa, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha chama kina miradi katika kila ngazi ili kujiendesha kikamilifu.

Katibu huyo ameeleza kuwa ujenzi wa ukumbi huo unasimamiwa vizuri chini ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi, na kamati ya ujenzi inayoongozwa na Mwita Gachuma.

Nashukuru ndugu mwandishi kwa kutembelea hapa ofisini na kuona maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano unaoendelea.

Ujenzi unaendelea vizuri kama ulivyoona, na huu ni uwekezaji unaotokana na maelekezo ya chama ngazi ya taifa. Baada ya kupokea maelekezo hayo, tulianza mara moja ujenzi huu,” amesema.

Amesema kuwa licha ya hatua kubwa zilizofikiwa, michango ya wanachama bado inahitajika ili kukamilisha hatua mbalimbali za ujenzi zilizobakia.

Aidha, ameongeza kuwa ukumbi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu na kuanza kutoa huduma. Michango ya vifaa na fedha bado inakaribishwa kupitia ofisi yake, huku kukiwa na namba maalum kwa ajili ya mfuko wa uchangiaji wa miradi ya chama. Amewashukuru wale wote waliochangia kufanikisha ujenzi huo hadi kufikia hatua ya sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!