Home Kitaifa TMA YATOA TAARIFA MWELEKEO MSIMU WA MVUA ZA MASIKA MACHI- MEI,2025

TMA YATOA TAARIFA MWELEKEO MSIMU WA MVUA ZA MASIKA MACHI- MEI,2025

Na Magrethy Katengu–Dar es salaam

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema Mvua za Masika zinatarajiwa kuanza mwezi Machi 2025 katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua, hususani maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, Pwani ya Kaskazini, na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.

Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt.Ladislaus Chang’a wakati akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam nakubainisha kuwa mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa kunyesha katika maeneo mengi ya Pwani ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa Victoria, na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.

Dkt.Chang’a amesema kuwa mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki pamoja na maeneo ya mashariki mwa Mikoa ya Simiyu na Mara.

Aidha ameongeza kuwa mwelekeo wa mvua za Masika 2025, kwa kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) pamoja na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma, Mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa, ambapo zitaanza Machi, wiki ya kwanza hadi ya pili, na kuisha Mei, wiki ya

Amesema Pwani ya Kaskazini (kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba) Mvua za wastani hadi chini ya wastani zitaanza Machi, wiki ya kwanza hadi ya pili, na kuisha Mei, wiki ya tatu hadi ya nne.

Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro), kutakuwa na Mvua za wastani hadi juu ya wastani ambapo zitaanza Machi, wiki ya pili hadi ya tatu, na kuisha Mei, wiki ya kwanza.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo wa TMA amesema kuwa athari zinazotarajiwa ni pamoja na unyevu na mafuriko, ambapo Mvua nyingi zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo, na huenda zikapelekea mafuriko na kuathiri ukuaji wa mazao.

Ameongeza kuwa kuhusu Maji, Kina cha maji katika mito na mabwawa kinaweza kuongezeka, na hivyo hatari ya mafuriko inaweza kujitokeza.

Ametahadharisha Magonjwa ya mlipuko yanaweza kutokea kutokana na uchafuzi wa maji unaoweza kusababisha magonjwa ya mripuko.

Amefafanua kuwa taarifa hiyo inatolewa kwa ajili ya kusaidia wadau wa sekta mbalimbali, kama vile kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili, afya, nishati, usafirishaji, na usimamizi wa maafa, kuchukua tahadhari stahiki na kupanga mikakati ya kukabiliana na athari za mvua.

Hata hivyo awali Dkt Chang’a amesema kuwa Mwenendo wa mvua za Msimu (Novemba 2024 – Aprili 2025) zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Singida na Dodoma, huku mvua za wastani hadi juu ya wastani zikitarajiwa katika mikoa ya Njombe, Ruvuma, Mtwara, Lindi na mikoa mingine kusini.

Hata hivyo amesema taarifa hiyo inatoa mwanga wa jinsi mifumo ya hali ya hewa itakavyokuwa kwa maeneo mbalimbali, kusaidia wahusika kupanga na kufanya maamuzi bora.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inawashauri watumiaji wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni wanashauriwa kuwasiliana na Mamlaka ili kupata taarifa mahsusi za utabiri wa msimu ili
kukidhi mahitaji maalum katika sekta zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!