Home Kitaifa JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM LAWAKAMATA WATUHUMIWA WA MAUAJI YA MZEE...

JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM LAWAKAMATA WATUHUMIWA WA MAUAJI YA MZEE REGINA CHAULA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili, Fredy Rajab Chaula na Bashiru Richard Chaula, kwa tuhuma za kula njama ya mauaji ya Regina Rajab Chaula (62), mkazi wa Bahari Beach, Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambaye pia ana makazi nchini Denmark.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake leo, Januari 20, 2025, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro, alisema mauaji hayo yametokea wakati marehemu alikuwa akifuatilia kesi zake za madai dhidi ya watuhumiwa hao, ambazo zinashughulikiwa na Mahakama Kuu, Divisheni ya Haki, jijini Dar es Salaam.

Mwili wa Regina Rajab Chaula, aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Desemba 13, 2024, uligunduliwa Januari 18, 2025, majira ya saa 8:00 mchana ndani ya nyumba yake.

Wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa kupotea kwa mama huyo, tulibaini shimo kubwa la maji machafu lililojengewa ndani ya nyumba yake. Tulilazimika kulibomoa na ndipo mwili wa marehemu ulipogunduliwa,” alisema Kamanda Muliro.

Jeshi la Polisi limekemea vikali kitendo hicho cha kikatili na kinyama kilichofanyiwa marehemu, huku likiahidi kuhakikisha wote waliohusika kwa namna yoyote katika mauaji hayo wanakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Kamanda Muliro ameongeza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria kwa wakati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!