Home Kitaifa RAIS SAMIA: “TUACHE MAZOEA, TUWASIKILIZE WANANCHI”

RAIS SAMIA: “TUACHE MAZOEA, TUWASIKILIZE WANANCHI”

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekemea na kutoa onyo kali kwa viongozi na makada wa CCM kuacha kufanya kampeni za mapema za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo ubunge. Amesema kuwa CCM ina ushahidi wa picha za wanaofanya hivyo.

Mwenyekiti Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akizungumza na wajumbe kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika jijini Dodoma leo, tarehe 18 Januari 2025, na kuendelea kesho tarehe 19 Januari 2025.

Masuala ya kampeni za mapema, nawaasa wale wanaojipanga kugombea, tunayakemea. Tayari tumepokea malalamiko na ushahidi wa picha za watu wanaofanya misafara kwenda majimboni, watu wanaoitisha mikutano mikuu ya majimbo kwa kisingizio cha ufugaji au mambo mengine, lakini dhamira yao ni kujitambulisha kwa wanachama,” alisema Dkt. Samia.

Tuna ushahidi wa picha nyingi sana. Sasa, tunaomba tutoe onyo mapema. Pia, viongozi na watendaji wa chama tuache kufanya kazi kwa mazoea. Niwaombe viongozi wa CCM msikilize wananchi na kero zao,” aliongeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!