Home Kitaifa DKT.MWINYI AELEZA MAFANIKIO YA ZIARA YAKE NCHINI OMAN

DKT.MWINYI AELEZA MAFANIKIO YA ZIARA YAKE NCHINI OMAN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, pamoja na ujumbe wake wamewasili katika uwanja wa ndege wa Sheikh Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Nchini Omani baada ya Kuhitimisha Ziara yake ya Kikazi ya Siku Nne.

Amepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais Hemed Seleman Abdullah, Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, Wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama wa SMZ, Viongozi wa dini.

Rais Dk. Mwinyi amezungumza na Wana habari mara baada ya kuwasili akitokea Ziara nchini Oman, amegusia mambo mbalimbali katika mazungumzo kati yake na mwenyeji wake mtawala wa Oman Mhe.Sultan Haitham bin Tariq na ziara yote kwa ujumla.

Amesema katika mkutano huo amepata fursa ya kuwaelezea hali ya utulivu ilivyo Zanzibar na kuwataka kuwekeza kutokana na kuwa ni wakati mzuri sasa kufanya hivyo.

Rais Dk. Mwinyi ameelezea mafanikio yaliyopatikana kwa Zanzibar kutokana na ziara yake katika nchi ya Oman aliyoifanya hivi karibuni aliyoianza Oktoba 11 mwaka huu na kuhitimisha tarehe 14 Oktoba.

Ameyataja mafanikio hayo ni ushirikiano wa eneo la elimu, ujenzi wa kituo cha data, Uhifadhi wa nyaraka za historia na ukusanyaji wa ushuru kupitia mfumo wa mtandao.

Rais Dk. Mwinyi amesema ametumia ziara yake hiyo kuelezea vivutio vya uwekezaji vilivyopo Zanzibar kwa wafanyabiashara wa Oman.

Pia, amesema katika ziara yake hiyo amewahakikishia wafanyabiashara wa Oman mazingira ya usalama katika uwekezaji Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!