Home Kitaifa WANAFUNZI SHULE YA WASICHANA JANGWANI WAPATIWA ELIMU YA USALAMA MTANDAONI

WANAFUNZI SHULE YA WASICHANA JANGWANI WAPATIWA ELIMU YA USALAMA MTANDAONI

Na Magrethy Katengu.

Serikali kipitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknilojia ya Habari imewashauri wanafunzi kutumia mitandao vizuri kuepuka kutuma ujumbe au picha zisizo na maudhui mazuri ili kuepukana na athari pale wanapotafuta fursa ikiwemo ajira au udhamini wa kuendelea na masomo

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha usalama Mtandaoni Wizara ya Habari, Mawasiliano Teknolojia ya Habari Mhandisi Steven Wangwe wakati wa akitoa elimu katika shule ya wasichana Jangwani iliyopo Dar es salaam ikiwa ni wa kampeni ya Duniani kuadhimisha juu ya usalama mtandao

“Usalama wa mtandaoni huaza na mtu binafsi hivyo tumeanza kutoa elimu katika kundi hili la wanafunzi mapema ili kuwanusuru wasije wakapoteza fursa za kielimu,kiajira zilizopo mbele yao kwani kupitia mtandao watu hufuatilia mtu anachokifanya bila yeye kujua hivyo amewasisitiza kuwa makini na maudhui ya mtandaoni”amesema Mhandisi Wangwe.

Hata hivyo amesema sasa hivi kumezuka mtindo wa watu kujipatia fedha kupitia mtandao kwa kufuatilia mtu kupitia simu yake na kuiba ikiwemo video au picha kisha kutishia kumdhalilisha kwa kutuma mtandaoni na kudai pesa ili asitume hivyo tunawapatia elimu mapema wanafunzi namna ya kuseti simu zao na kuzitumia ili hali hiyo isije ikawagharimu. ..

Kwa upande wake mwalimu wa shule ya sekondari ya Wasichana Jangwani Salum Kilipamwambu pia Mratibu Shule mtandao iliyopo chini ya Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema wao wanatoa elimu lakini walimu walio wengi hawana elimu ya usalama wa mtandao kwani wanakaa na Jamii inayowazunguka na huku wanatumia baadhi ya vitu lakini hawavifahamu usalama wa mtandaoni vitu hivyo, hivyo Serikali iliangalie hilo kwa jicho la tatu

“Wanafunzi hawa pamoja na kusoma mambo ya darasani lakini wanatakiwa waielewe Dunia ya Ulimwengu wa teknolojia ikoje kwani kwa sasa wanasoma kompyuta,wanatumia simu na kutumia vifaa mbalimbali vya tehama hivyo wasipojua namna ya kuvijua hasara na faida zake”alisema Mwalimu.

“Somo la teknolojia ya habari na Mwasailiano(TEHAMA) shuleni linafundishwa lakini halipewi kipaumbele katika ufundishwaji ,hivyo tunaiomba serikali itilie mkazo somo hili muhimu kwa wanafunzi ili wajue mapema matumizi sahihi ya mtandao”amesema Mwalimu Kilipamwambu.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliyopewa elimu juu ya matumizi usalama mitandao akiwemo Anna Ngowi ambaye anasoma kidato cha 6 shuleni hapo amesema hatua ya Wizara ya habari kutoa elimu hiyo ni yakuungwa mkono kwani imewapa elimu nzuri juu ya jinsi gani wataepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

“Kwa sisi wanafunzi tunashukuru kwa kupewa elimu hii,na tumejifunza ni vitu gani vya kuposti na visivyo vya kupost mitandaoni ili visitudhalilishe na kupelekea kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji wa kimtandao (cyber bullying)hivyo nawaomba vijana wenzangu hasa wanafunzi watumie vyema mitandao”amesema Neema Matilda ambaye ni wanafunzi wa kidato cha 5 shuleni hapo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!