Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi wa Kongamano la Nishati safi ya Kupikia yaani ‘Clean Cooking Conference‘ ili kuchunguza vikwazo vinayodumaza matumizi ya nishati za kisasa za kupikia.
Kongamano hilo linalenga kupendekeza mikakati ya kufanikisha upatikanaji wa nishati safi, za bei nafuu na endelevu nchini Tanzania.
Mkutano huo utafanyika tarehe 1 na 2 Novemba 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha watunga sera, wadau wa maendeleo, wajasiriamali, wawekezaji, wafadhili, wanataaluma na wananchi kwa ujumla.