KAMPUNI ya Cocacola wazindua rasmi Kampeni ya chipsika kiajira na Cocacola ambapo Vijana 300 katika wilaya zote za Jijini la Dar es salaam kushikwa Mkono kwa kupatiwa vitendea kazi.
Akizungumza na waandishi wahabari octoba 11 Jijini Dar es salaam,Meneja Masoko na Mahusiano wa Kampuni ya Cocacola Victor Amos amesema Kampeni hiyo inalenga kuwashika mkono vijana katika Wilaya za Jijini Dar es salaam ikiwemo Kinondoni,Ilala,Temeke,Kigamboni ili kuboresha biashara zao na kuwapa elimu namna ya kufanya biashara ya chips.
Aidha,Amos ameeleza kuwa kwa sasa Kampeni hiyo Ina lengo la kuwakwamua kiuchumi wajasiriamali hususani vijana wa kitanzania mkoa wa Dar es salaam na kwa sasa Washiriki wanaruhusiwa kutuma maombi ili Kamati ya timu ya Kampeni hiyo kuchunguza vigezo vya kukidhi kushiriki.
“Fomu zinazopatikana ofisini Mikocheni kiwanda cha cocacola, mtandaoni kwenye kurasa za cocacola hivyo washiriki hasa wapishi wa chips wanaruhusiwa kuanzia kushiriki Huku vigezo na masharti kuzingatiwa ikiwemo mshiriki awe kuanzia miaka 18 mpaka 35,awe raia wa Tanzania,awe na vitambulisho vya kiraia.”
Pia ameeleza kuwa Shindano hilo linatarajiwa kufanyika octoba 29 mwaka huu Huku maombi ya ushiriki yakifikia kikomo octoba 26 mwaka huu .
Hata hivyo Kwa upande wa Mdhamini wa Shindano hilo kutoka Kampuni ya M_Gas Meneja Mauzo na Maendeleo Nelson Chusi amesema Kwa kushirikiana na Cocacola wameamua kuungana nao ili kuwawezesha vijana kuendana Mabadiliko ya nishati ya gesi katika matumizi mbalimbali ikiwemo kupika Ili kutunza Mazingira na kuacha Kabisa matumizi ya mkaa.
“Kupitia huduma ya M_gas inawezesha watumiaji na hata wajasiriamali kujua Salio lililobakia kwenye mtungi pamoja na kununua gesi kwa kima cha chini shilingi elfu 1 kulingana na matumizi yake.”
Hata hivyo ameongeza kuwa katika Kampeni hiyo watatoa jiko la gesi pamoja na vifaa vyote kwa washindi wa Kampeni hiyo kama sehemu ya kuunga Mkono na kuwanyanyua vijana kiuchumi Huku Elimu ya namna gani matumizi ya M_gas itakavyotunza vipato vyao kupitia huduma mbalimbali ikiwemo mkopo wa gesi kwa gharama ya shilingi elfu 40.