Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amewasili jioni hii katika uwanja wa ndege wa Entebbe Uganda kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za miaka 60 ya Uhuru wa Uganda.
Dk Mwinyi katika ujumbe alioambatana nao yupo Mama Mariam Mwinyi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Mbarouk Nassor.
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe, Rais Dk. Mwinyi amepokelewa na Mnadhimu Mkuu wa Serikali katika Bunge la Uganda Obua Hamson pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Dk Aziz Ponary Mlima.
Sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Uganda zitafanyika kesho Jumapili tarehe 09 Oktoba 2022 katika viwanja vya sherehe Kololo..