Serikali nchini Tanzania imepokea wawekezaji kutoka nchi za falme za kiarabu wenye nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha mazao mbali mbali
ikiwemo kilimo cha Parachichi katika mkoa wa Njombe.
Mbunge wa Afrika Mashariki Bi, Fancy Nkuhi akiiwakilisha nchi ya Tanzania amesema wawekezaji hao wamewasili nchini na kufika katika mkoa wa Njombe kwa nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha Parachichi huku akibainisha kuwa ugeni huo ni matunda ya ziara ya Rais Samia aliyoifanya nchini Oman wiki mbili zilizopita.
Kwa mujibu wa kampuni ya BACOIN ya nchini Tanzania iliyofanikiwa kufika
na wawekezaji hao mkoani Njombe imebainisha kuwa nia ya wawekezaji hao sambamba na kilimo cha Parachichi ni kufanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa kiwanda cha Nyama huku katika sekta ya utalii wakiwa na malengo ya ufugaji wa farasi.