NA BONIFACE GIDEON, TANGA
MASHINDANO ya kutafuta vipaji vya mchezo wa Ngumi Mkoa wa Tanga Maarufu kama Five Brothers boxing championship yameanza kupata mwitikio mkubwa wa Mashabiki ikiwa ni Msimu wake wa pili toka kuanzishwa kwake.
Mashindano ya Boxing ambayo yameandaliwa na kudhaminiwa na kampuni ya Burudani Jiji Tanga ya Five Brothers
Entertainment ikiwa na Lengo la kutoa na Kuongeza Hamasa ya mchezo wa ngumi Kwenye Jamii na Kutoa Fursa kwa Mabondia wachanga wenye Ndoto za Kupanda Ulingoni na Kupambania mikanda mbali mbali Wapate nafasi Ya Kuonyesha vipaji vyao kwenye mchezo huo ili Mabondia hap waweze kutimiza ndoto Zao.
Mkurugenzi wa Five Brothers Nasor Makau aliwaambia Waandishi wa Habari Jana kuwa
“Tunamalengo ya kufanikisha ndoto kwa mabondia Wachanga na hii itawawezesha kufikia malengo yao walio jiwekea na Kufufua matumaini yaliyo ndani ya mchezo wa boxing” Alisema Nasor
Alisema Mashindano hayo yalianza Rasmi kwa mara ya kwanza July 2021 kwa Kuzunguka maeneo mbalibali ya Jiji la Tanga ambapo zikiwamo kata za Chumbageni,Magomeni Magaoni Makorora na kumalizikia Katika uwanja wa Mkwakwani,
“Tarehe 24 mwezi wa September mwaka huundio tumefanya uzinduzi wa msimu wa Pili mwaka huu na tarehe 4 mwezi huu tulienda kata ya Mwanzange katika Uwanja wa CCM na Leo hii tupo kata ya Ngamiani kusini tukiendelea kutafta vipaji na muitikio wa Wananchi ni mkubwa” Alisisitiza Nasor Makau
Mwisho