Home Kitaifa TARI YATATHIMINI MAFANIKIO YAKE, TEKNOLOJIA YAPEWA KIPAUMBELE

TARI YATATHIMINI MAFANIKIO YAKE, TEKNOLOJIA YAPEWA KIPAUMBELE

Na. BONIFACE GIDEON, Tanga

Wstalaamu kutoka TARI Kanda ya Mashariki inayojumuisha Mikoa ya Tanga, Pwani na Dar es Salaam wamekutana kwa Siku mbili Jijini Tanga Oktoba 3-4 kwa Lengo la kujadili Tathmini na mafanikio waliyoyapata kwa kipindi Cha mwaka 2021/2022 pamoja kusambaza Teknolojia na kuweka mikakati zaidi ya Utafiti ambao unaendelea katika Vituo vya Tari Mlingangano, Tari Kibaha na Dar es Salaam, Mkutano huo umejumuisha Wataalamu mbalimbali kutoka katika Vituo Vitatu vinavyounda Kanda hiyo ya Mashariki.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mkurugenzi wa Kituo Cha TARI Mlingano kilichopo Wilayani Muheza Mkoani Tanga Dkt. Catherine Senkoro Alisema TARI inamajukumu makubwa mawili ambayo ni kufanya Utafiti na kusambaza Teknolojia iliyofanyiwa Utafiti.


TARI inamajukumu makubwa mawili ambayo ni kufanya Utafiti na kusambaza Teknolojia ambayo tunaifanyia Utafiti kwa Wananchi na tumeyatekereza hayo yote kwa Muda muafaka na kwenye kwenye kikao hiki tunajadili Yale ambayo tumeyatekereza kwenye kipindi Cha mwaka 2021/2022 na tunafanyaj Tathmini ya Utafiti wetu ndio Mana tupo na Wataalamu ” Alisema Dkt. Catherine

Alisema TARI Mlingano imefanikiwa kufanya Utafiti juu ya zao la Mkonge na kupata Matokeo makubwa ikiwamo Dawa za Kutibu Magonjwa na Wadudu wanaoshambulia zao Hilo pamoja na Aina Bora za Mbegu,

Baadhi ya Magonjwa yanayoshambulia Mkonge ni pamoja na kuoza kwa Shina, Ugonjwa wa Pundamilia , Ugonjwa wa Madoa Doa lakini pia Kuna Wadudu hatari Sana wanaoshambulia zao Hilo ambao wanaitwa Mgongo wa Tembo ambao hushambulia moyo wa Mkonge” Alisisitiza Dkt.Catherine

Alisema Mkulima anatakiwa kuwasiliana na Wataalamu wa Kituo hicho au kufika kwenye Kituo ili upate Ushauri wa Kitaalamu na wao wanatoa Ushauri pamoja na Teknolojia ikiwamo uuzaji wa Mbegu Bora za Mkonge ,

“Mwaka huu tumevuka lengo la kuzarisha Miche ya Mkonge ambapo Wakulima wameshainunua Miche yote Mil.3 na Bado wanahitaji hivyo kwa muitikio huu huenda tukavuka lengo la kuzarisha Miche Mil.10 kwa Mwaka kabla ya mwaka 2025 kama inavyoelekeza Sera ya Taifa na sisi Kama Kituo tumejipanga kuvuka lengo kabla ya hapo” Alisisitiza Dkt. Catherine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!