Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,Mhe Mohamed Mchengerwa leo Oktoba 4, 2022, ametembelea eneo mashuhuri la uigizaji wa filamu nchini Uturuki chini ya mwongozaji mahiri wa filamu Mehmet Bosdaq, Bosdaq Film.
Mehmet na kampuni hiyo ndio wazalishaji wa filamu mashuhuri zinazorushwa nchini za Dirilis Ertugrul na Kurulus Osman (the Ottoman).
Katika ziara hiyo ambayo wamekubaliana kushirikiana kusaidia kuinua sekta ya filamu nchini Tanzania, Mhe Waziri ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Balozi Lt. Generali Yacoub Mohammed na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi.