Na Magreth Mbinga
Mradi wa Tanzania Agrobusiness Window umeweza kupatia fedha kampuni 50 ambazo zinajishughulisha na maswala ya kilimo hapa Nchini ambapo mradi huo unalenga wakulima wadogo pamoja na kutoa huduma ya mbegu bora na kuweza kununua mazao ya wakulima pamoja na kuwapatia masoko bora.
Hayo yamesemwa na Meneja wa aecf hapa Tanzania Gerald Mgesi katika mahojiano na mwandishi wetu na kusema kuwa mradi umetekelezwa Nchini Tanzania kwa thamani ya zaidi ya Dola Milioni 38 ambazo zimwtolewa na Serikali ya Uingereza na Sweden .
“Mradi umekuwa ukitekelezwa hapa Nchini na shirika la aecf lililoanzishwa mwaka 2007 na mradi umeanza kuleta mabadiliko makubwa kwenye jamii tumeweza kupikia watu zaidi ya lakin 5 imeweza kuongeza kipatao takribani zaidi ya Dola 137 ikilinganishwa kabla ya mradi haujaanza” amesema Mgesi.
Pia Mgesi amesema sehemu kubwa ya mradi kwa mara ya kwanza ilikuwa ni kutoa uelwwa kuhusu kilimo hasa mbegu bora,matumizi sahihi ya virutubishi pamoja na mahitaji yanayoweza kutumika katika uzalishaji.
“Kampuni ambazo tumezipatia fedha kwa kiasi kikubwa zilikuwa zinaanza na kutoa elimu kwa wakulima kabla ya kuweza kutumia watu wetu kuweza kupeleka huduma maeneo ya mbali ambapo huduma zilikuwa haziwezi kufika kwa kiasi kikubwa” amesema Mgesi.
Aidha Muendesha Miradi Agrobusiness Sebastian Wanjala amesema wana sherehekea mafanikio ya kampuni na kuona hali ya mradi Nchini Tanzania miaka 10 iliyopita kampuni iliwekeza ela na wametoa fursa kwa wakulima wadogo.
“Changamoto kubwa katika huu mradi ni baadhi ya sekta binafsi ambazo zipo Afrika hazina njia ya kupatia masoko sisi tunajaribu kutatua changamoto hizo kwa kuangalia kivipi tunaweza kuwatafutia masoko ambayo yanaweza kukidhi mahitaji ya bidhaa zao” amesema Wanjala.