Na Magrethy Katengu
Shirika la reli Tanzania – TRC limezindua mafunzo kwa vitendo kwa watendaji wa TRC yatakayotolewa na wataalamu kumi na watano (15) kutoka Shirika la Reli la Korea – KORAIL, katika ukumbi wa mikutano makao makuu TRC jijini Dar es Salaam Septemba 28, 2022.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa amesema mafunzo haya ni utekelezaji wa mkataba wa mafunzo kwa vitendo uliosainiwa tarehe 4 Julai 2022 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani Ikulu Jijini Dar es Salaaam kati ya TRC na KORAIL.
“Haya ni maandalizi ya uendeshaji wa treni ya kisasa ambayo miundombinu yake kwa kipande cha kwanza cha Dar es Salaam hadi Morogoro imekamilika kwa zaidi ya asilimia 97 na kipande cha pili kutoka Morogoro hadi Makutopora kimekamilika kwa zaidi ya asilima 91” amesema Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Kadogosa.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Kadogosa amesema Shirika limeamua kuwatumia KORAL kutoa mafunzo kwa vitendo kwa watendaji wa TRC kwasababu uendeshaji wa treni ya kisasa Korea ya Kusini ni salama kwa asilimia 99.9, hii inaonesha wana wataalamu waliObobea katika nyanja zote za uendeshaji wa treni ya kisasa.
Baadhi ya nyanja ambazo wataalamu wa KORAIL watatoa mafunzo ya nadharia na vitendo ni jinsi ya kupanga treni, uongozaji wa treni, uendeshaji wa treni, biashara ya treni, kutoa utaalamu wa karakana ziweje na usafirishaji katika uendeshaji wa treni. Mafunzo yatakuwa ni ya kina nayatatolewa kwa muda wa miaka mitatu.
“Ili kupata elimu nje ya muda wa kazi ni vyema kuwa na uhusiano mzuri na wataalamu hawa kutoka KORAIL kwa sababu watakuwa TRC kwa muda mrefu” amesisitiza Ndugu Kadogosa.
Mkurugenzi Mkuu TRC ametoa ufafanuzi kuwa uendeshaji wa treni ya kisasa utaanza rasmi mwezi Februari 2023 baada ya taratibu zote za majaribio kufanyika na kukubaliana gharama za usafirishaji na Mamlaka ya Udhibiti Usafi Ardhini – LATRA.
Naye Meneja wa mradi kutoka KORAIL Lee Seung Young ameshukuru uongozi wa TRC kwa kuwaamini kwa kazi ya utaoaji mafunzo kwa vitendo katika uendeshaji wa treni ya kisasa na kuahidi kutoa mafunzo kwa ufanisi kwasababu wamekuja na wataalamu katika nyanja mbalimbali na wana uzoefu wa kutosha kwenye uendeshaji wa treni ya kisasa.
Mafunzo kwa vitendo kwa uendeshaji wa treni ya kisasa yatashirikisha watendaji vijana zaidi ya thelathini kutoka TRC na wataalamu kumi na tano kutoka KORAIL., katika ukumbi wa mikutano makao makuu TRC jijini Dar es Salaam Septemba 28, 2022.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa amesema mafunzo haya ni utekelezaji wa mkataba wa mafunzo kwa vitendo uliosainiwa tarehe 4 Julai 2022 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani Ikulu Jijini Dar es Salaaam kati ya TRC na KORAIL.
“Haya ni maandalizi ya uendeshaji wa treni ya kisasa ambayo miundombinu yake kwa kipande cha kwanza cha Dar es Salaam hadi Morogoro imekamilika kwa zaidi ya asilimia 97 na kipande cha pili kutoka Morogoro hadi Makutopora kimekamilika kwa zaidi ya asilima 91” amesema Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Kadogosa.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Kadogosa amesema Shirika limeamua kuwatumia KORAL kutoa mafunzo kwa vitendo kwa watendaji wa TRC kwasababu uendeshaji wa treni ya kisasa Korea ya Kusini ni salama kwa asilimia 99.9, hii inaonesha wana wataalamu waliObobea katika nyanja zote za uendeshaji wa treni ya kisasa.
Baadhi ya nyanja ambazo wataalamu wa KORAIL watatoa mafunzo ya nadharia na vitendo ni jinsi ya kupanga treni, uongozaji wa treni, uendeshaji wa treni, biashara ya treni, kutoa utaalamu wa karakana ziweje na usafirishaji katika uendeshaji wa treni. Mafunzo yatakuwa ni ya kina nayatatolewa kwa muda wa miaka mitatu.
“Ili kupata elimu nje ya muda wa kazi ni vyema kuwa na uhusiano mzuri na wataalamu hawa kutoka KORAIL kwa sababu watakuwa TRC kwa muda mrefu” amesisitiza Ndugu Kadogosa.
Mkurugenzi Mkuu TRC ametoa ufafanuzi kuwa uendeshaji wa treni ya kisasa utaanza rasmi mwezi Februari 2023 baada ya taratibu zote za majaribio kufanyika na kukubaliana gharama za usafirishaji na Mamlaka ya Udhibiti Usafi Ardhini – LATRA.
Naye Meneja wa mradi kutoka KORAIL Lee Seung Young ameshukuru uongozi wa TRC kwa kuwaamini kwa kazi ya utaoaji mafunzo kwa vitendo katika uendeshaji wa treni ya kisasa na kuahidi kutoa mafunzo kwa ufanisi kwasababu wamekuja na wataalamu katika nyanja mbalimbali na wana uzoefu wa kutosha kwenye uendeshaji wa treni ya kisasa.
Mafunzo kwa vitendo kwa uendeshaji wa treni ya kisasa yatashirikisha watendaji vijana zaidi ya thelathini kutoka TRC na wataalamu kumi na tano kutoka KORAIL.