Machifu kutoka mkoa wa Mara wamezungumza na Waandishi wa Habari kuhusu matukio ya mauaji yaliyotokea mkoani Mara.
Tamko hilo limetolewa tarehe 28 Septemba 2022 kwa niaba ya Machifu wa Mkoa wa Mara na Chifu Japhet Wanzaji (Chifu wa Himaya ya Zanaki) la kumpongeza Chifu Hangaya pamoja na Jeshi la Polisi chini ya IGP Camillius Wambura, baada ya kuona jitihada zao za kuhakikisha ulinzi na usalama katika mkoa wa Mara na taifa kwa ujumla.
“Sisi umoja wa Machifu mkoani Mara leo tarehe 28 September 2022, baada ya kumaliza kikao cha pamoja kilichojadili hali ya kiulinzi na kiusalama wa mkoa wetu wa Mara, tunapenda kumpongeza Chifu Hangaya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na IGP Wambura kwa jitihada zao za kuhakikisha ulinzi na usalama wa mkoa wa Mara na Taifa kwa ujumla”
Pia kwa niaba ya Umoja wa Machifu wa mkoa wa Mara, Chifu Japhet Wanzaji wa Himaya ya Zanaki, wanaliomba Jeshi la Polisi liendelee na Operesheni hizi za kuzuia uhalifu katika mkoa wa Mara na nchi nzima ili watanzania na Taifa kwa ujumla kuwe na ulinzi na usalama.
“Sisi kama viongozi wa kimila tunaomba kuendelea kufanya operesheni kama hizi ili kuzuia uhalifu nchi nzima”
Mwisho Viongozi wa kimila walitoa wito kwa watanzania kuendelea kudumisha Amani ya nchi yetu
“Tunaomba tutoe wito kwa wakazi wa Mara na watanzania wote kuendelea kudumisha Amani ya nchi yetu”