Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa leo Septemba 26, 2022 amewasili Mkoani Manyara na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Manyara, Mhe. Charles Makongoro Nyerere kwa ziara ya Kikazi ya siku mbili mkoani humo.
Bashungwa ameambatana na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Charles Msonde na anatarajia kuwa na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika sekta za Elimu, Afya, barabara na Utawala katika wilaya ya Hanang’, Mbulu Mjini na Mbulu Vijijini mkoa huo.