Na Mwandishi Wetu, TANGA
MASHINDANO ya Kutangaza Utalii wa Ndani yamefana mkoani hapa Baada ya kuwavutia Watu mbalimbali wa Ndani na nje,
mashindano hayo ya Majahazi yanayotumia Upepo bila kutumia mafuta na kuhimili baharini yakiwa na Abiria 50 yamefana na
Majahazi hayo 24 yalianzia Visiwani Zanzibar kuelekea katika hifadhi ya Taifa ya Saadan mkoani Tanga ikiwa na lengo kuu la kutangaza utalii wa ndani.
Mashindano hayo yanafanyika kila mwaka yanayoratibiwa na Dar es salaam yach club kwakushirikiana Mataifa Mbalimbali Duniani.
Kiongozi wa msafara huo Roland Vandeven amesema mashindano hayo ni Mara ya pili kufanyika toka kuanzishwa kwake na matarajio yao mwakani mashindano hayo yawe ya kidunia.
Pia Roland amefurahi kufikia katika hifadhi ya Taifa ya Saadan kwakuwa yatahamasisha watalii wa ndani na nje kwenda kutembelea hifadhi hiyo.
Kwa upande wake kamishina msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Eprahim Mwangomo amesema kuwa mashindano hayo yatasaidia kufungua fursa mbalimbali, na kuzitangaza fursa hizo zilizopo katika hifadhi ya Taifa ya saadan ili kuendelea kuvutia Watalii kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo watalii wa ndani nje.
Mashindano hayo yalianzia Jijini Dar es salaam na kuelekea stone town Zanzibar – Saadan na kisha kuelekea Gezira Gungu ambapo watakaa siku tano na yatamalizika msasani jijini Dar es salaam .