Home Kitaifa WATOTO WALIOIBIWA WAKUTWA KWA MGANGA WA KIENYEJI

WATOTO WALIOIBIWA WAKUTWA KWA MGANGA WA KIENYEJI

Na Magrethy Katengu
Dar es salaam

Watoto wawili Mahdy Kasim(me) Umri 04 na Husna Kasim(ke) 05 walioibiwa na binti wa kazi za ndani Januari 11, 2025 Tandika Temeke wamepatikana nyumbani kwa Mganga wa kienyeji Abdulkarim Sharif (43)huko Kimara Baruti Ubungo Januari 14, mwaka hui

Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi WA habari leo Januari 15, 2025 Kamanda wa polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam SCP Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi lilipokea taarifa ya tukio la kupotea watoto hao Januari 12 mwaka huu ndipo walipoanza upelelezi mara moja na kuwa tukio hilo lilitendwa na binti wa kazi za ndani kwa kushirikiana na Mganga wa kienyeji ambapo walipanga njama na kuona watoto hao lakini mpango wao uligonga Mwamba baada ya kupatikana kwa watoto hao ndani ya siku chache.

“Tumewafanyia vipimo vya Hospitali watoto hawa na kubaini afya zao ni nzuri na tunaendelea na mahojiano ya kina na Watuhumiwa yakikamilika na kubaini nini kiini na malengo ya tukio hilo wote waliohusika watafikishwa kwenye Mamlaka zingine za kisheria haraka iwekezanavyo kwa hatua zaidi huku dada wakazi ambaye hajulikani alipo juhudi zikifanyika za kumtafuta” amesema Kamanda

Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es salaam linatoa wito kwa wananchi kuepuka tabia ya kuchukua wasaidizi wa kazi za nyumbani wasiowajua historian zao wala tabia kwani kufanyia hivyo ni hatari iliyojificha inaweza kuwaathiri wenyewe.

Katika tukio lingine Jeshi la Polisi linawashikilia Watuhumiwa ambapo ni Askari wawili wa kikosi cha Usalama Barabarani ambao picha yao mjongeo ilikuwa ikitembea katika mitandao ya kijamii ikiwaonyesha wakipokea rushwa kitendo ambacho ni kinyume maadili kinachafua taswira ya Jeshi la Polisi.

“Askari hao tayari tumeshawakamata wapo mahabusu na hatua Kali za kinidhamu za mashtaka ya kijeshi zimeanza kuchukuliwa kabla ya hatua nyingine za kisheria kuchukuliwa

Sambamba na hayo Jeshi la Polisi Kanda Maalumu litaendelea kuchukua hatua kali na za haraka na halitavumilia kitendo vyovyote vya kulidhalilisha Jeshi vilivyo kinyume na maadili ya Jeshi au kuchafua Taswira ya serikali na kinyume cha Sheria za nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!