Home Kitaifa WANACHAMA WA CCM WATAKIWA KUJIEPUSHA NA MAJUNGU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

WANACHAMA WA CCM WATAKIWA KUJIEPUSHA NA MAJUNGU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

NA WILLIUM PAUL,

WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi wameshauriwa kujiepusha na maneno ya uongo (majungu) hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ili chama hicho kiingie katika uchaguzi wanachama wakiwa wamoja na kuweza kushinda kwa kishindo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Meryse Mollel wakati akifunga baraza la Umoja wa Wanawake wa chama hicho, (UWT) wilaya ya Moshi vijijini ambapo alisema kuwa, wapo watu ambao kazi yao ni kueneza uongo ili kuwafarakanisha wanachama na viongozi wao.

“Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu hivyo wanaccm tunawajibu wa kuhakikisha tunasimama wamoja na kuepuka maneno maneno ya uongo na ya uchonganishi tusije kuingia katika chaguzi tukiwa tumepasuka makundi makundi” Alisema Meryse.

Katibu huyo alisema kuwa, chama hicho kimeshinda kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana na hii ni kutokana na ushirikiano na umoja uliokuwepo baina ya viongozi na wanachama.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM wilaya ya Moshi vijijini, Ramadhani Mahanyu alitumia nafasi hiyo kuwaonya baadhi ya viongozi pamoja na wanachama ambao wameanza kuwapitisha wale wenye nia ya kugombea badae mwaka huu na kudai kuwa kwa sasa chama kinawatambua viongozi waliopo madarakani.

“Mwanachama tutakayembaini ameanza kujipitisha huko na kuwavuruga viongozi waliopo madarakani tutawachukulia hatua kwa mujibu wa chama chetu waacheni viongozi waliopo wafanye kazi zao na muda wa kampani utakapofika tutawapima kulingani na kazi zao” Alisema Mahanyu.

Aidha Katibu huyo aliwataka wanaccm kuwasemea mazuri yale yote yaliyofanywa na viongozi ikiwemo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa wananchi ili wasipotoshe na wale wasiokitakia mema chama cha Mapinduzi

.Katika hatua nyingine aliupongeza Umoja wa Wanawake wilaya ya Moshi vijijini kwa jinsi walivojitoa kuhakikisha chama kinashinda katika uchaguzi wa serikkali za mitaa na kuwaomba nguvu na umoja huo kuuamishia katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Naye Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Moshi vijijini, Ruaichi Kaale alitumia nafasi hiyo kuwasihi Wanawake kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi pindi muda utakapofika ili kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Alisema kuwa, wakinamama ni jeshi kubwa linalotegemewa na CCM kuhakikisha wanambeba Rais Samia katika uchaguzi wa mwaka huu na kuwaomba kuhakikisha anapata kura za kishindo katika wilaya hiyo.

“Rais Samia ameonyesha mwelekeo bora kwa sisi wakinamama kuwa tunaweza kuongoza sasa ni kipindi chetu sisi kumuunga mkono kwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi lakini pia kumtafutia kura za kishindo na hili ni jambo ambalo tunaliweza” Alisema Ruaichi .

Kwa upande wake Katibu wa UWT wilaya ya Moshi vijijini, Oliver Ngalawa alisisitiza juu ya uhai wa Jumuiya pamoja na chama ikiwa ni pamoja na ulipaji wa ada, kuingiza wanachama wapya pamoja na vikao vya kikanuni na kufanya ziara mbali mbali za kutoa elimu juu ya uhai wa jumuiya

Katika Baraza hilo waliwatunuku vyeti vya pongezi na zawadi mbalimbali kwa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi vijijini, Wabunge wa majimbo na viti maalum mkoa, pamoja na Kata zilizofanya vizuri kwenye zoezi la usajili wa wanachama wa UWT sambamba na ulipaji wa Ada.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!