Na Ashrack Miraji Fullshangwe Media
Vijana Askari 80 wa jeshi la Akiba (mgambo) wamehititimu mafunzo yao ya miezi minne yaliyofanyika katika kata ya Bombo, Tarafa ya Gonja Wilaya ya Same, askari hao wamekula kiapo cha utii kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari kufanya kazi kwa kujitolea kulitumikia Taifa kama walinzi wa usalama wa raia na mali zao.
Akihitimisha mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amawataka kutumia mbinu walizofundishwa kwa manufaa ya jamii, hususani kulinda raia na mali zao, kuzingatia matumizi sahihi ya Silaha Pamoja na mbinu mbalimbali walizojifunza na kuepuka kujihusisha na matukio ya uhalifu.
Aidha amewasisitiza askari hao kwamba Pamoja na wajibu wao wa msingi kwnye masuala ya usalama, askari hao ni kiungo muhimu kuhamasisha uzalendo kwenye jamii, kuunganisha Serikali na jamii hasa panapohitajika ushiriki wa raia katika shughuli za kijamii za kujitolea Pamoja na kuchangia miradi ya maendeleo hasa nguvu kazi.