Na Shomari Binda-Musoma
MCHANGO wa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo ukiwemo wa kifedha na kutafuta kura kwenye uchaguzi umempa tuzo kutoka jumuiya ya wazazi ya CCM.
Katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika hivi karibuni Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Musoma vijijini imetambua mchango wa mbunge huyo.
Kwenye kikao cha baraza la jumuiya hiyo kilichofanyika Kijiji cha Murangi wajumbe walitoa tuzo hiyo iliyokabidhiwa na Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM mkoa wa Mara Simon Rubugu aliyekuwa mgeni rasmi wa baraza hilo.
Akikabidhi tuzo hiyo ya pongezi Rubugu amesema jumuiya ya wazazi imefanya jambo jema katika kutambua mchango wa viongozi katika kushiriki kwenye matukio mbalimbali yakiwemo ya uchaguzi.
Amesema mchango wa mbunge Profesa Sospeter Muhongo umeoneka na kupelekea chama kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi uliofanyika novemba 27.
Rubugu amesema Muhongo alipita kuelezea wananchi (wapiga kura) mafanikio makubwa ya serikali inayoongozwa vizuri na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na utekelezaji wa ilani jimboni na kutaka kuichagua CCM.
Mwenezi huyo wa CCM mkoa wa Mara amesema mbunge Muhongo licha ya kushiriki kampeni alichangia uchapishaji na ugawaji wa vitabu viwili vya rangi (Volumes III & IV) vinavyoelezea miradi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM jimboni nakala elfu moja na mia tano (1,500).
Aidha kutoa posho za mawakala wakati wa upigaji kura za maoni ndani ya chama matawi 95, usafiri kwenye kampeni za wagombea wa CCM nafasi za serikali za Vijiji 68,usafiri wa wapiga kampeni wakiwemo viongozi watatu kutoka kila Kata mambo ambayo yanastahili pongezi.
Amesema katika uchaguzi wa Vijiji 68 CCM ilipata viti 66 (97.06%), CHADEMA 2
na Vitongoji 374: CCM ilipata 358 (95.72%), CHADEMA 16 ambao ni uehindi wa kishondo.