Na Mwandishi Wetu.
Kuelekea Sherehe za Krismas na Mwaka Mpya Kampuni ya Ukopeshashaji wa Mikopo ya OYA MICROFINANCE imeamua kurudisha kwa jamii kwa kutoa misaada kwa vituo vya watoto yatima na watu wenye mahitaji maalum katika mikoa ambayo wanatoa huduma nchi nzima
Akizungumza Mkurugenzi wa OYA Mr. Alpha Peter akiwa kwenye moja ya kituo cha watoto yatima cha Magomeni Dar es salaam amesema
” Jamii nzima ya OYA, uongozi na wafanyakazi imeona ni vyema kuendelea kurudisha upendo kwa jamii zetu zoote za Tanzania.
Na msimu huu wa mwisho wa mwaka ni msimu wa kufurahi na wale wote tuwapendao. Hivyo basi hatuna budi kujumuika pamoja na Watoto hawa wenye uhitaji mkubwa sana wa upendo wa hali na mali.
Tumeona ni vyema kufurahi pamoja na kuzishukuru jamii zetu kwa ujumla kwa kuendelea kutuamini sisi na kushirikiana pamoja kwenye kuijenga Tanzania iliyo bora zaidi. Tumechangia mahitaji muhimu kwa vituo takribani 20 vinavyolelea watoto yatima na wenye mahitaji maalumu kwenye Mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Kahama, Geita na Mara.
Tunashukuru sana jamii nzima ya Tanzania na serikali yetu kwa kuweka mazingira Rafiki ya kufanya biashara kwenye jamii zetu.
Kwa pekee nawashukuru sana wateja wetu woote ambao ndio sehemu kubwa ya mafanikio ya OYA na pia wafanyakazi wetu wote na uongozi kwa kuwa wao ndio nguzo pekee ya mafanikio yetu. Jamii zetu zoote zilizopo kwenye mikoa tunayofanya biashara tunawashukuru saana na tunaomba waendelee kutuamini na sisi tutafanya jitihada zoote kuhakikisha tunachochea maendeleo yetu pamoja “