Home Kitaifa DKT. BITEKO ATOA WITO WAKUKUZA UBUNIFU WA NDANI KWA MAENDELEO YA TAIFA

DKT. BITEKO ATOA WITO WAKUKUZA UBUNIFU WA NDANI KWA MAENDELEO YA TAIFA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa pamoja na jitihada za kuwainua wabunifu wawekezaji nchini, bado kuna umuhimu mkubwa wa kuwawezesha wabunifu wetu kukua zaidi ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Desemba 16, 2024 Jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la Uwekezaji wa Kampuni Bunifu (STARTUPs)

Amesema kuwa Tanzania imerekebisha mifumo mingi ili kuwezesha ubunifu na uwekezaji wa moja kwa moja nchini kuleta maendeleo, suala ambalo tumeona likifanikiwa na kwahiyo linahitaji kupaliliwa na kuungwa mkono kwa matokeo chanya.

Nimewasikiliza wanakongamano na kupitia majadiliano haya ni wazi kwamba bado kuna namna ya kuboresha zaidi mifumo yetu ya usimamizi na utawala ili kuhakikisha Wabunifu wanapata nafasi nzuri zaidi.” amesema na kuongeza kuwa, Tunatamani kuona Watanzania wanashiriki katika kukuza uchumi wa nchi yao na pengine kuazimwa katika nchi nyingine.” amesema Dkt. Biteko

Amesema wapo baadhi ya Watanzania wanaofanya shughuli zao nje ya Nchi ambao wanaiwakilisha vema Tanzania kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia misingi iliyowekwa katika nchi hizo na hivyo kuwataka wabunifu wawekezaji kuiga mfano huo.

Aidha, Dkt. Biteko amesema kuwa Maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yako wazi na kwa nyakati mbalimbali amekuwa akijipambanua kuhusu uwezeshaji wa makundi mbalimbali wakiwemo wabunifu wawekezaji.

kwa kutekeleza maono ya Rais, ni muhimu kuwasikiliza, kuwaamini na kufanyia kazi maoni na bunifu zao ili kuboresha mazingira yatakayo wawezesha kutekeleza Bunifu zao na kupata fursa ndani na nje ya Nchi”.

Naye, Naibu Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo akimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Kitila Mkumbo amesema Serikali imekuwa ikizingatia suala la uwezeshaji kwa Wabunifu Wawekezaji ikiwa ni pamoja na kupokea maoni yao kupitia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Nyongo ameongeza kuwa, Serikali imeboresha mazingira ya biashara kwa kupunguza gharama za biashara ili kuwawezesha wabunifu kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wake, Waziri Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa amesema Wizara imeandaa mazingira ya kuwawezesha Wabunifu kufanya majaribio ya kazi zao kupitia mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Amesema Serikali imejenga vituo vya ubunifu vinane (8) katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kuwawezesha Wabunifu kujiandaa na hatimaye kupata ajira katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TSA, Zahoro Muhaj amemshukuru Rais Samia kwa maono yake ya kuwatambua na kuwawezesha wabunifu ili waweze kuchagiza maendeleo ya nchi.

Tunaomba salam zetu zifikishwe kwa Mheshimiwa Rais, ambaye amekuwa akitubeba na kusafiri nasi katika nchi mbalimbali ili tupate uzoefu na kukua kama mtu kama mtu mmoja mmoja na baadae kama Taifa,” amesema Muhaj.

Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Nelson Bonephace ameishukuru Serikali kwa jitihada za kuwawezesha wabunifu wawekezaji kukua.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2020 hadi sasa zaidi ya dola za kimarekani Milioni 49 zimetolewa ambazo zinatumika kujenga Kampasi mpya za Kagera, Zanzibar na Lindi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!