Na Magrethy Katengu
Tanzania yawekeana Saini na nchi Jamhuri ya Kidemokrsai ya Kongo(DR CONGO) katika Makubaliano ya ushirikiano wa kuboresha sekta ya ulinzi ikiwa ni sehemu ya kuendeleza mahusiano mema yaliyopo baina ya Mataifa hayo.
Mara baada ya zoezi la kusaini hati ya makubaliano Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nchini Tanzania Stergomena Tax amesema zoezi la makubaliano limeanza baada mazungumzo ya kamati ya ushirikiano sekta ya ulinzi JPC ambapo utakuwa wa kudumu
Hata hivyo Waziri amesema makubaliano hayo ni mwendelezo wa ushirikiano wa kuimarisha sekta ya ulinzi ya Tanzania na DR Congo ili kuwa na mwambata wa wanajeshi yaani Tanzania kupokea wanajeshi kutoka DR Congo huku DR Congo ikipokea wanajeshi kutoka Tanzania kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
“Makubaliano haya yanalenga kuboresha maeneo mbalimbali katika sekta ya ulinzi ikiwemo kubadilishana taarifa za kiintelejensia,kufanya kwa pamoja mafunzo na mazoezi ya kijeshi na kitaalamu, kutembeleana ‘ kushirikiana katika masuala ya maafa,pia kushirikiana katika tiba wakati wa oparesheni mbalimbali kuwakamata wahalifu wanaovuruga amani” amesema Waziri Stergomena
Sambamba na hayo Waziri ameongeza Kwa kusema kuwa hakuna maendeleo bila amani hivyo Tanzania na DR Congo zinahitaji kuimarisha biashara na vichocheo vingine akitolea mfano miundombinu ya barabara pamoja na bandari huku akisihi DR Congo kuwa sehemu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa DR Congo Gilbert Kabanda Kurhenga amesisitiza kuendeleza mahusiano mazuri kati ya Taifa lake na Tanzania huku akiwa na imani kuwa kupitia makubaliano hayo ya kuboresha sekta ya ulinzi itasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na vitendo vya uhalifu
” Leo ni siku ya furaha kwetu kukutana katika mkutano huu na kusaini hati ya makubaliano ya kuimarisha sekta ya ulinzi kwa mataifa yetu ambayo yamekua kama ndugu kufuatia ushirikiano wetu wa muda mrefu, hivyo naamini tutaendeleza uhusiano wetu na tutaboresha sekta ya ulinzi pamoja na mambo mengine muhimu kwa mataifa yetu ” amesema Kurhengau..