Home Kitaifa RAIS SAMIA AELEKEA BLAZIL KUSHIRIKI MKUTANO WA G20

RAIS SAMIA AELEKEA BLAZIL KUSHIRIKI MKUTANO WA G20

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tarehe 16 Novemba, 2024 kabla ya kuelekea Rio de Janeiro nchini Brazil kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa kundi la G20. Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Brazil Mhe. Luiz IÅ„acio Lula da Silva ambapo pamoja na mambo mengine, atashiriki mijadala inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa na umasikini, kuchochea maendeleo endekevu na matumizi ya nishati mbadala.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!