Na Magrethy Katengu
Jamii, taasisi za serikali, binafsi na mashirika mbalimbali yameombwa kujali kundi la watoto waishio mazingira hatarishi kwa kuwajali kwa namna yeyote kwani wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali, kukosa mahitaji muhimu ikiwemo chakula mavazi, malezi Ili kusaidia nao wajisikie vizuri licha ya kifo kuwatenganisha na wazazi wao .
Ushauri huo umetolewa Jijini Dar es salaam katika makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani Diwani wa kata ya Kawe, Mutta Rwakatale ambapo alisema kwa kutambua kuwa kuna umuhimu wa kuonyesha upendo wa dhati hivyo wanatarajia kuungana na Mkuu wa Jeshi la Polisi ‘IGP’ Camilius Wambura katika siku maalum ya watoto yatima inayoandaliwa na kituo cha Voice of Orphans Tanzania
Diwani Rwakatare amesema siku hiyo inaandaliwa na kituo hicho kikiwa na kauli ya “Mikononi mwa polisi yatima wapo salama” lengo ni kuwafanya yatima nchi nzima wajihisi salama.
“Nilipewa wazo na kituo cha Voice of Orphans Tanzania niliamua kulibeba kwakuwa niliona ni jambo zuri nikiwa kama diwani, na kuomba wakuu wa jeshi la polisi mikoani kote kutumia siku hiyo kwa ajili ya kula na yatima“.amesema Diwani
“Tumemfikishia IGP Wambura na ametukubalia, na tutakula naye siku hiyo wakati wa kuonesha kwamba watoto yatima wapo mikononi salama katika mikono ya jeshi la polisi” amesema Rwakatale.
Mkurugenzi wa kituo hicho Maria Msaada amesema viongozi wote wa polisi katika mikoa yao watakuwa wanakula pamoja.
“Malengo ni kuonesha watoto yatima wapo salama mikononi mwa polisi, lakini pia kuwafanya watoto yatima wanapopata matatizo wawe wanakimbilia polisi” alisema.