Home Kitaifa SHULE YA SEKONDARI MISUFINI GOMA KUANZA KUPOKEA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO...

SHULE YA SEKONDARI MISUFINI GOMA KUANZA KUPOKEA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO 2025.

Zaidi ya shilingi milioni 389 kutumika kujenga Mabweni mawaili (KE&ME), vyumba vinne vya madarasa na matundu ya vyoo kumi na nne (14) katika Shule ya Sekondari Misufini Goma iliyopo Kata ya Ndungu Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni maandalizi ya kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka 2025.

Akizungumzia ujenzi huo Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Adam Agustino alisema ujenzi huo unakwenda sambamba na ujenzi wa nyumba ya walimu (two in one) kwa gharama ya shilingi milioni 98 na utekelezaji wake umefikia hatua ya kupandisha tofali. Huku ujenzi wa vyumba vya madarasa umefikia hatua ya renta, Mabweni yapo hatua ya msingi, na mafundi wapo wanaendelea na ujenzi.

Jitihada za Serikali za kuboresha mazingira ya elimu zinamfanya Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni kufanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo kukagua utekelezaji wa miundombinu hiyo, ambapo alisistiza mafundi kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi kukamilisha ujenzi kwa wakati ili ifikapo 2025 wanafunzi wa kidato cha tano waanze kupokelewa.

“Tunaishukuru sana Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya elimu kwa vijana wetu, lakini pia kwa walimu, kwa kiasi kikubwa miundombinu ya elimu kwenye Wilaya yetu inazidi kumalika sana”. Alisema DC Kasilda.

Aidha ujenzi huo ni sehemu ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu ya Shule hiyo mpya ambayo awali Serikali ilitoa zaidi ya shilingi milioni 580 ambazo zilitumika kujenga miundombinu ya jengo la utawala, vyumba nanne vya madarasa vyenye ofisi mbili za walimu, matundu kumi (10) ya vyoo (KE &ME), majengo matatu ya maabara (Physics, Chemistry na Biology), jengo la maktaba pamoja na la Tehama.

Utekelezaji wa shule hiyo uliibuliwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya Sekondari Ndungu lakini pia kuondoa adha kwa watoto waliokuwa wakilazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa saba kutoka Kijiji cha Misufini hadi shule ya Skondari Ndungu.

Shule ya Sekondari Misufini Goma tayari imeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!