Home Kitaifa WALIOLETA NYUKI UWANJANI WALIWA KAMA ASALI.

WALIOLETA NYUKI UWANJANI WALIWA KAMA ASALI.

TERMINAL FC MABINGWA WA MATHAYO CUP MANKA FC WALOA TEPETEPE DK 90.

na Dickson Mnzava, Same .

Timu ya vijana wa stand wilayani Same Mkoani Terminal FC wamenyakua kombe la MATHAYO CUP 2024 baada ya kuingushia mvua ya magoli 4-1 vijana Kutoka milima ya mshewa Manka FC maarufu kwa jina la wazee wa kuleta nyuki uwanjani.

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Kata ya kisiwani wilayani Same Mkoani Kilimanjaro na kushudiwa na mamia ya washabiki wa mchezo wa soka Kutoka Kata mbalimbali ndani ya Wilaya hiyo ya Same.

Manka FC walikuwa wa kwanza kupata goli la uongozi dk huku kipindi cha kwanza kikimalizika kwa Manka wakiwa wanaongoza goli moja kwa bila kipindi cha pili kiliaanza kwa kasi ambapo terminal FC vijana wa stand wilayani walisawazisha goli hilo dakika ya na kuwaduwaza Manka FC.

Haikuchukua dakika nyingi terminal FC kuandika goli la pili nakuzima kelele za mashabiki wa Manka FC dk ya …na goli la tatu dakika ya ….ndoto za Manka FC zilizimwa dakika ya… baada kufungwa goli la nne na hadi mwamuzi wa mchezo huo …anapuliza kipenga cha mwisho vijana wa stand wilayani Same terminal FC goli 4 Manka FC 1.

Baada ya mchezo huo mdhamini wa mashindano hayo David Mathayo Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi amesema mashindano hayo ni endelevu na lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji vya soka kwa vijana wa Jimbo la Same Magharibi sambamba na kutengeneza fursa za ajira kwa vijana hao.
“Kwanza niwashukuru sana wananchi wa Same hususani Jimbo hili la Same Magharibi kwakujitokeza kwa wingi sana kwenye uwanja wa kusiwani lakini pia niwapongeze washindi wote kuanzia mshindi namba moja hadi mshindi wa nne ambao wote wamepata zawadi hii leo kubwa zaidi niwapongeze vijana wa stand Same terminal FC kwakunyakua kombe la MATHAYO CUP hakika kila mmoja ameweza kujionea fainali ya aina yake yenye vipaji na ubunifu mkubwa mno katika soka”

“Aidha nisemetu mashindano haya ni endelevu na msimu unaokuja dau la zawadi litaongezeka zaidi Kutoka milioni 7 kwa mshindi wa kwanza hadi milioni 10 hivyo niwakati wa vijana kuendelea kujifua ili waweze kupata nafasi ya kujitangaza kwenye mashindano haya”
“Alisema mheshimiwa mbunge Mathayo David “.

Hata hivyo katika fainali hiyo mshindi namba moja alijinyakulia kombe lenye thamani ya laki tano,pesa taslimu milioni 7,seti ya jezi na mpira pamoja na medali kwa wachezaji na viongozi wa timu, mshindi wa pili ameondoka na milioni 5 jezi, mpira na medali kwa wachezaji na viongozi mshindi wa Tatu amejinyakulia milioni 3.5 jezi pamoja mpira na medali kwa wachezaji na viongozi huku mshindi wa nne alijinyakulia kitita cha milioni 1.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!