Home Kitaifa DKT BITEKO ; IFIKAPO 2030 BARA LA AFRIKA WATU MILLION 300 WATAFIKIWA...

DKT BITEKO ; IFIKAPO 2030 BARA LA AFRIKA WATU MILLION 300 WATAFIKIWA NA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Na Magrethy Katengu– Dar es salaam

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishato Dkt Doto Biteko amesema Bara la Afrika linaendelea kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha ifikapo 2030 takribani watu million 300 wamefikiwa na nishati ya safi ya kupikia

Ameyasema hayo leo Oktoba 16, 2024 Jijini Dar es salaam katika Jukwa la.majadiliano kuhusu nishati safi ya kupikia bara la Afrika lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na , lengo ni kujadiliana na kubadisha na uzoefu juu ya upatikanaji wa Nishati safi ya kupikia ambapo mfumo wake unachangamoto nyingi kwenye utekelezaji wake ikiwemo gharama ya upatikanaji.

“Watu wengi wanalalamika gharama ni kubwa ya kupata huduma hiyo, sasa ni lazima kuweka mikakati mizuri ili kuhakikisha gharama za upatikanaji wake uwe rahisi na watu waweze kumudu, huku mitungi ya gesi laki 4 itapangwa kuuzwa kwa nusu bei”amesema Dkt Biteko

Dkt Biteko amesema Jukwaa hilo pamoja na mambo mengine litakua ni maandalizi ya mkutano wa wakuu wa nchi wa Afrika wanaokwenda kujadili masuala ya nishati kwenye bara la Afrika kwani watu 300 sio kazi rahisi kuwapata.

Amesema kuwa, Benki ya maendeleo ya Afrika imepima kwa vipimo vyake kwa kukaa na wadau wote ambao wanapata pesa kutoka kwao imeonekana Tanzania imepiga hatua kubwa na wamefanikiwa jambo lililopelekea nchi hiyo kuwa shamba darasa kwa nchi jirani kwenye usimamizi wa Sekta ya nishati.

” Nchi ya Tanzania imepata heshima ambayo haikua kazi rahisi bali ni moja mausiano mazuri ya kidiplimasia kati ya nchi hiyo na Benki ya maendeleo ya Afrika ambapo wamekiri Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye masuala ya kisera na usimamizi, uzalishaji na usafirishaji na upelekaji wa umeme Vijijini” amesema Naibu Waziri Mkuu

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Nishati, mabadiliko ya tabia nchi na ukuaji wa kijani AFDB Dr Kelvin Kairuki amesema wameamua kufanya kazi pamoja na Tanzania kwa sababu ipo mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira

“Tanzania imekua ikitilia manani mambo ya nishati safi ndio sababu tutakuwa tukiwasadia kufikia afua zao walizojiwekea hivyo kama World Benki tukasema hili kongamano lifanyike Tanzania kwani kupata watu million 300 wa kutumia nishati safi ya kupikia sio rahisi” amesema Dr Kairuki.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Eng Felchesmi Mrama amesema mkutano huo wataweza kujadiliana ukuaji wa Nishati, matarajio, namna ya kupata uzalishaji na ujumuishaji wa Sekta binafsi kwani ifikapo 2034 nishati ipatikane kwa unafu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!