Home Burudani MOUNT MERU MARATHON YAANZA KUJIPANGA AFCON 2027 KWAKUTANGAZA FURSA ZA KIUCHUMI.

MOUNT MERU MARATHON YAANZA KUJIPANGA AFCON 2027 KWAKUTANGAZA FURSA ZA KIUCHUMI.

Na Boniface Gideon, TANGA

Waandaji wa mashindano ya Mount Meru Marathon yanayotarajiwa kufanyika Novemba 3 mwaka huu katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, wamesema kwasasa wameanza maandalizi ya AFCON 2027 kwakutangaza fursa mbalimbali za kiuchumi na Utamaduni Mkoa wa Arusha,

Mwandaaji wa mbio hizo Dinna Mosha aliwaeleza Waandishi wa Habari hivi karibuni kuwa ,kuwa kuelekea michuano hiyo mikubwa barani Africa ,wameamua kutangaza utamaduni wa Tanzania kuanzia vyakula na Lugha.

Akiwa mkoani Tanga mara baada ya kukutana na wadau mbalimbali Dinna alisema kuwa kutokana na maendeleo ya teknolojia na uttandawazi kwaa sasa kuna hatari ya kupoteza na kusahauu asili za kimakaanila huasusani kwa kwa kizazi kijacho hivyo kupitia tamasha hilo itakuwa njia ya kuwakumbusaha wzazi , walezi na jamii kwa ujumla kusimamia majukumu yao kwa watoto.

“Tumekuja hapa Tanga kutangaza fursa,tunataka tupate watu wa mapishi,wanaopika vyakula vya kitanzania,tutawashindanisha siku hiyo,haya yote tunayafanya ili kutangaza fursa kuelekea michuano ya AFCON 2027″Alisema Mosha

Alisema kuwa wameamua pia kumnusuru kijana wa kiume ili kujenga Taifa imara lenye vijana wenye uzalendo na Nchi yao,

” Tumeamua kumnusuru kijana wa kiume,huyu ndiyo kichwa cha familia lakini pia huyu ndiyo anayeongeza ukoo wa familia na Taifa kwa ujumla,tunatoa Elimu ya Makuzi na kuwajengea uwezo Vijana kuwa wazalendo na Nchi yao” Aliongeza Mosha

         MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!