Home Kitaifa AMANI NA UTULIVU NCHINI NI MSINGI WA BABA WA TAIFA HAYATI MWALIMU...

AMANI NA UTULIVU NCHINI NI MSINGI WA BABA WA TAIFA HAYATI MWALIMU NYERERE – DKT KIKWETE

RAIS Mstaafi wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema amani na utulivu ambayo nchi nyingi duniani na bara hili wanayaona nchini ni matokeo ya msingi imara ambao umejengwa chini ya uongozi wa Baba taifa hayati Mwalimu Julias Nyerere na kuongeza kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kulinda na kuenzi.

Ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la Maadhimisho ya Kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere chini ya kaulimbiu “Mwalimu Nyerere na Vuguvugu la Ukombozi: Tafakari Mshikamano, Uongozi, Pan-Africanism na Umoja wa Afrika”, iliyofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere ya Mjini Kibaha mkoani Pwani.

Alisema moja ya njia sahihi ya kumuenzi Muasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ni kwa kutekeleza kwa vitendo aliyoyafanya wakati wa uhai wake kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali hususani katika uongozi.

“Mwalimu alikuwa mtu wa aina hiyo ambaye aliishi maneno yake na alijitolea maisha yake kwa ajili ya maisha ya watu wachache”.

“Hatuwezi kuzungumza juu ya uhuru na maendeleo katika eneo hili la Afrika bila kumtaja mtu huyu ambaye bado tunayo mengi ya kujifunza. kutoka, na njia pekee ya kumtukuza ni kufanya yale aliyotufundisha wakati wa uhai wake,” alisema.

“Leo, tumekusanyika hapa, watu kutoka nchi mbalimbali kutafakari maisha ya kiongozi wetu ambaye aliuthibitishia ulimwengu kwamba binadamu wanaweza kuishi kwa kuheshimiana na kwamba ubaguzi wa rangi, ukoloni mamboleo na aina zote za dhuluma za kijamii zinaweza kupigwa vita tu. ya watu kufanya kazi chini ya umoja na dhamira”, alieleza.

Dkt. Kikwete alisema pia tunachakujifunza kwa Baba wa taifa ni alikuwa mzarendo wa Kweli mwenye kuamini katika misimamo yake ambayo hakukatishwa tamaa Wala kuvunjwa Moyo katika harakati za kupigania uhuru wa nchi yetu licha ya kupitia changamoto mbalimbali ikiwemo kushitakiwa, kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa kulipa faini sambamba na kudhihakiwa na wakoloni kwaajili ya kupigania uhuru wa nchi yetu.

“Nyerere alipitia mengi huku wakimuhoji na kumtaka achague kuendelea na ajira yake ya ualimu ambayo ilikuwa na mshahara au ataendelea na harakati zake za kupigania uhuru wa nchi yetu”

Akizungumzia umuhimu na sababu za kuanzishwa kwa Shule ya uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere Dkt Kikwete alisema ni lengo la kuwajengea uwezo wa kada mbalimbali za uongozi kutoka Vyama sita rafiki ambayo ni CCM, FRELIMO, ANC, ZANU PF, SWAPO na MPLA kwa ushirikiano wa Chama Cha kikomunisti Cha nchini China CPC.

Aidha aliwataka viongozi kuondoa dhana ya kwamba Shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere ni ya Chama Fulani Bali ni ya Vyama vyote sita rafiki vya harakati za ukombozi.

Hatahivyo alisisitiza viongozi ambao wamepewa mamlaka ya kusimamia Shule kuendelea kuitunza miundombinu ya shule hiyo na Rasilimali zote za shule zilizopo.

Prof. Marcellina Chijoriga- Mkuu wa Chuo hicho alisema katika salamu zake za ukaribisho kwamba Doalogue iliandaliwa hasa kwa ajili ya kuenzi maisha ya Hayati Mwalimu Nyerere na pia kutumia fursa hiyo kujadili michango yake katika ukombozi wa Bara la Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!