Home Kitaifa DC SAME AONGOZA WANANCHI KATIKA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA MAKAZI

DC SAME AONGOZA WANANCHI KATIKA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA MAKAZI

Na Ashrack Miraji Same Kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amesema zoezi la Undikishaji Wananchi kwenye Daftari la Mkazi linaendelea vizuri, Wananchi wamehamasika vituo vingi wameshajiandikisha na bado wanaendelea kujiandikisha.

DC Kasilda amezungumza hayo Oktoba 11 mwaka huu 2024 mara baada ya kujiandikisha katika daftari la mkazi kwenye Kitongoji Stesheni Kilichopo Kata ya Stesheni ambacho ni miongoni mwa kituo cha uandikishaji Wananchi kwenye Daftari la Mkazi kati ya vituo 503 vilivyopo Wilayani humo.

Aidha amesisitiza Wananchi wakazi wa Same kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vilivyopo kwenye maeneo yao kujiandikisha ili wawe na uhalali wa kupiga kura Novemba 27 mwaka huu 2024.

“Tayari kama Mkuu wa Wilaya nimejiandikisha, lakini pia nimepata nafasi ya kukagua baadhi ya vituo kuona hili zoezi linaendaje, nimefarijika sana zoezi linaendelea vizuri Wananchi wamehamasika vituo vingi wameshajiandikisha na bado wanaendelea kujiandikisha”. Alisema DC Kasilda.

Zoezi la Uandikishaji wananchi kwenye daftari la mkazi limeanza rasmi leo Oktoba 11 na linaendelea hadi kufikia Oktoba 20 mwaka huu 2024.

Kauli mbiu “Serikali za Mitaa, Suti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!