Home Kitaifa DC KUBECHA AMEONGOZA KAMPENI YA HAMASA YA USHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA...

DC KUBECHA AMEONGOZA KAMPENI YA HAMASA YA USHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

Na Ashrack Miraji

Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe Japhari Kubecha Jana Tarehe 9 Oktoba ,2024 Amezindua Kampeni Kabambe ya Kuhamasisha Wananchi Kushiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Pamoja na Ushiriki wa Kujiandikisha kwenye Orodha ya Daftari la Wapiga ni muhimu Kwa maslahi mapana ya Taifa letu

“Nawaomba wananchi wote kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huu kwa lengo la kuchagua viongozi watakaoliletea taifa letu tija na maendeleo,” alisema Kubecha

Kampeni hiyo ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa Barozi Batilda Burihani amesema nampongeza Mkuu WA Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha, Kwa kuendelea kuwa mbunifu kuhasisha vijana kushiriki katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kwani kampeni hii inalenga kuimarisha umoja wa Watanzania bila kujali tofauti za dini, kabila au itikadi za kisiasa.hapa Nchin

Uzinduzi huo ulifanyika katika Kata za Mabawa na Msambweni, ukihimiza umuhimu wa kulinda demokrasia kupitia vyama mbalimbali na kuchagua viongozi wenye nia ya kweli ya kuleta maendeleo kwa wananchi.

Kampeni hiyo pia iliambatana na burudani kutoka kwa wasanii maarufu akiwemo Kiredeo, Wazee wa Makoti na vikundi vingine vya burudani, vilivyochangamsha wananchi waliojitokeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!