Na Boniface Gideon, TANGA
Mkuu wa wilaya ya Tanga Japhari kubecha amewataka wananchi wa jiji la Tanga kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa,hivi karibuni uandikishaji kwa wapiga kura wapya na maboresho ya ya taarifa kwenye daftari la mpiga kura litaanza rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Japhari Kubecha,amewaeleza Waandishi wa Habari jana kuwa, Uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu nakwamba utatanguliwa na matukio mbalimbali ikiwamo zoezi la maboresho na uandikishaji kwa wapiga kura wenye sifa zakupiga kura,
“Kabla ya Uchaguzi huu kufanyika Novemba 27 mwaka huu,kutakuwa na matukio mbalimbali ikiwamo zoezi la maboresho ya taarifa kwa wale wapiga kura ambao walipiga kura lakini pia kuna waliohama vituo vyao vya makazi,kuna wapiga kura wapya nao pia wanatakiwa wakajiandikishe ili wapate sifa zakuwa wapiga kura” Alisisitiza Kubecha
Aliwataka watu wote wenye sifa zakuchagua na kuchaguliwa kujitokeza ili wapate fursa zakuchagua na kuchaguliwa,
“vyema wale wote wenye sifa za kushiriki zoezi hili,kutumiza haki yao kikatiba ya kuwachagua viongozi wanaowahitaji na kuchaguliwa,na hasa vinana wajitokeze kwa wingi kushiriki, vyama vya siasa vioo tayari kwa Uchaguzi hivyo ni fursa kwakijana mwenye sifa kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni Lakini pia kujiunga kwaajili ya kuchagua na kuchaguliwa” Aliongeza Kubecha
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amesema msingi wa uchaguzi mkuu ni uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo katika kuhakikisha wananchi wanapata viongozi bora ni vyema kujitokeza katika mikutano ya vyama vya kisiasa na kuskiliza pande zote ili kufanya maamuzi sahihi wakati wa zoezi la kupiga kura.