Home Kitaifa WANAMICHEZO WA MALIASILI WAPONGEZWA KWA KUTANGAZA UTALII KWENYE MASHINDANO YA SHIMIWI 

WANAMICHEZO WA MALIASILI WAPONGEZWA KWA KUTANGAZA UTALII KWENYE MASHINDANO YA SHIMIWI 

Na. John Bera

Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambao ni wanamichezo, wamepongezwa kwa jitihada zao za kuutangaza Utalii kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mkoani Morogoro

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bw. Benard P. Marcelline alipoitembelea kambi ya wachezaji hao mkoani Morogoro

“Nimekuja kuwasilimia na kuwapongeza, mmefanya kazi kubwa sana, mmeitangaza Wizara, mmeutangaza Utalii maana kila kona ni Maliasili, hongereni sana” amesema Marcelline.

Mkurugenzi huyo  amesema lengo la Wizara kuwaleta katika  Mashindano hayo, kwanza ni kushiriki, kuwawezesha watumishi hao kujumuika na watumishi wengine ili waweze kufahamiana na kubadilisha uzoefu pamoja kuutangaza Utalii 

Aidha, amewapongeza wachezaji hao kwa  kuweza kufuzu kuingia Fainali ya mbio za mita 100, 400 kwa upande wa wanawake  na 800 kwa upande wa wanaume ikiwemo na kuingia robo fainali kwenye Mchezo wa Kamba ( Ke) pamoja na Kamba (Me)

Bw. Marcelline, ametumia fursa hiyo kuipongeza Menejimenti ya Wizara kwa kuendelea kuiunga mkono na kuisimamia timu hiyo ili kuhakikisha inafanya vizuri 

Pia, ameupongeza uongozi wa timu hiyo kwa jitihada zao za kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri na kuiwezesha timu kufanikia hadi kufikia hatua hiyo 

Sanjari na hayo, Bw. Marcelline amezishukuru na kuzipongeza Taasisi za Wizara pamoja na Benki ya NMB kwa kuziwezesha timu hizo katika maeneo mbalimbali ikiwemo vifaa vya michezo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa timu hiyo, Bw. Gervas Mwashimaha amesema maendeleo ya timu hiyo ni mazuri na timu hiyo ina ari ya kufanya vzuri ndio mana wameweza kufanikiwa kufika robo fainali ya michezo hiyo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!