Home Kimataifa WAZIRI MKENDA AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA VENEZUELA MHE YURI

WAZIRI MKENDA AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA VENEZUELA MHE YURI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda jana tarehe 5 Septemba 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Venezuela Mhe Yuri Pimentel anayeshughulikia maswala ya Afrika.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam na kujadiliana kwa kina kuhusu mambo mbalimbali ya ushirikiano kwenye elimu, sayansi na teknolojia.

Mara baada ya mazungumzo hayo Waziri Mkenda alishudhudia utiaji saini ya makubaliano kati ya Tanzania na Venezuela kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, sayansi na teknolojia uliofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Balozi Liberata Mulamula na Naibu Waziri huyo wa Venezuela Mhe Yuri Pimentel anayeshughulikia maswala ya Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!