na Dickson Mnzava, Same.
Mbunge wa Jimbo la Same mashariki Anna kilango Malecela ametoa kiasi cha milioni moja kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa choo cha wanafunzi katika Shule ya Msingi Mroyo iliyopo katika Kijiji cha Mpirani kata ya Maore wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.
Mheshimiwa Anna kilango Malecela ametoa kiasi hicho mbele ya wananchi wa eneo hilo wakati akiwa kwenye ziara yake ya kutembelea wananchi kwenye tarafa zake zote kwaajili ya kusikiliza kero mbalimbali na kuzitatua huku akiwasihi wananchi kushiriki kwenye uandikishwaji wa daftari la makazi na kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Awali kwenye mkutano huo wa mheshimiwa mbunge na wananchi mwalimu Mkuu wa shule ya msingi mroyo Evaline Mkwema aliwasilisha kilio hicho cha ukosefu wa choo bora kwaajili ya wanafunzi ndani ya shule hilo kitu ambacho amesema kinahatarisha usalama wa afya kwa wanafunzi hao.
Mkwema amesema Shule hiyo ina wanafunzi wapatao 510 lakini pia wanakabiliwa na changamoto ya madarasa huku akiomba serikali kuweza kutatua changamoto hiyo.
Kufuatia kilio cha mwalimu huyo mbele ya mbunge wa Jimbo hilo Anna kilango Malecela ndipo mbunge alipotoa kiasi hicho cha milioni moja kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa choo hicho cha wanafunzi.
” Ndugu zangu wananchi wa mroyo twendeni tukakamilishe ujenzi wa choo hicho tukumbuke watoto ni wetu na wanatakiwa kukaa sehemu salama hivyo pamoja na mimi kutoa pesa hii lakini tushirikianeni katika kumaliza ujenzi wa choo hicho naamini baada ya kumaliza hili tutavuka hatua nyingine”
“Alisema Mama Anna kilango Malecela”.
Hata hivyo katika ziara yake hiyo pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua pia ameendelea kuhimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la makazi litakaloanza tarehe 10 mapema mwezi Octoba na kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mwisho.