Home Kitaifa RAC TANGA BATILDA BURIHANI ATOA WITO KWA WAKAZI WA TANGA NA WANANCHI...

RAC TANGA BATILDA BURIHANI ATOA WITO KWA WAKAZI WA TANGA NA WANANCHI KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII NCHINI

Na Ashrack Miraji Lushoto Tanga

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Batilda Burihani ametoa wito kwa wakazi Mkoani Tanga na watanzania kwa ujumla kujenga tabia ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini ikiwemo vivutio vya utalii vinavyopatikana Wilayani Lushoto ili kujifunza kuhusu historia, tamaduni na mazingira hatua itakayo wasaidia kupata fursa ya kupumzika, kufurahia uzuri wa asili na kukuza pato la Taifa.

RC Batilda ametoa wito leo 21 Septemba 2024 wakati akikagua maandalizi ya mwisho kuelekea kilele cha USAMBARA TOURISM FESTIVAL ambayo yanafanyika Wilayani Lushoto siku ya Jumapili ya 22 Septemba 2024 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Bitteko katika viwanja vya Nyerere Square.

Akiwa katika hifadhi ya msitu wa Magamba na vivutio vya Kiguluhakwewa Dkt. Batilda amesema Wilaya ya Lushoto ni moja ya maeneo yenye vivutio vizuri vya utalii na vyenye kutembelewa na wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani ambapo kwa mwaka jana inakadiriwa takribani watalii 5000 walitembelea Wialya hiyo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Zephania Summaye amezindua Ofisi ya Umoja wa Waongoza Watalii Lushoto ambapo ameahidi kuwa mlezi wa kituo hicho pia na amewataka kuongeza elimu na kuwa wakarimu kwa wageni wanao wapokea na kuwatembeza katika vivutio hivyo.

Awali wakisoma Risala yao mbele ya Mkuu wa Wilaya wameomba kutatuliwa kwa baadhi ya changamoto ikiwemo kutolewa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wautalii na kuwekomesha utaratibu wa baadhi ya wageni kutembelea vivutio bila kufuata utaratibu rasmi.


Tamasha la USAMBARA TOURISM FESTIVAL linalenga kuvitangaza vivutio vya utalii katika Wilaya ya Lushoto ambapo zitaambatana na mbio fupi kwa washiriki mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!