Home Kitaifa BUMIJA ASHINDA MWENYEKITI CHADEMA MKOANI PWANI

BUMIJA ASHINDA MWENYEKITI CHADEMA MKOANI PWANI

Mwandishi Wetu, Pwani
Septemba 9, 2024

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Pwani kimemchagua Bumija Moses kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano Njuweni, Kibaha Mjini Mkoani Pwani, ambapo msimamizi wa uchaguzi huo Katibu CHADEMA Kanda ya Pwani, Jerry Richard Kerenge alimtangaza Bumija kuwa mshindi nafasi ya Mwenyekiti mkoa kwa kupata kura 48 kati ya 87 zilizopigwa.

Jerry alieleza kura zilizopigwa ni 87 zilizoharibika ni 2 ambapo mshindi wa pili Iddy Msawanga alipata kura 33.

Alitaja pia nafasi ya Katibu ambayo ameshinda Richard Mbalase ambae amepata kura 48 na kumshinda Bosco Mfundo aliyeshika nafasi ya pili.

Jerry alieleza kuwa, walikuwa na muendelezo wa uchaguzi mikoa ya Pwani ambapo mkoa wa Temeke ameshinda Elman Kiloloma kwenye nafasi ya Mwenyekiti huku nafasi ya Katibu akichukua Emmanuel Sudai.

“Ngazi ya mkoa tumemaliza tunasubiria ngazi ya Kanda ambalo zoezi la kuchukua fomu limekoma tarehe 5 septemba”

Akijinasibu kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba mwaka huu na uchaguzi mkuu ujao, Jerry alifafanua mkakati wao kumaliza viporo kata na mitaa.

Alisema kuwa wamejipanga kusimamisha wagombea katika uchaguzi unaokuja na kushinda katika mitaa 640, vijiji 431 na vitongoji 1,789 vilivyopo Chadema ukanda wa Pwani unaohusisha mikoa Pwani, Ilala, Temeke, Ubungo na Kinondoni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!