Home Kitaifa BARAZA LA MADIWANI LUSHOTO HAWANA IMANI NA (NEMC) BAADA YA KUPEWA ELIMU...

BARAZA LA MADIWANI LUSHOTO HAWANA IMANI NA (NEMC) BAADA YA KUPEWA ELIMU YA MADINI YA BAUXITE

Mwenyekiti wa Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Mathew Paul amesema Elimu iliyotolewa na nemc kama Baraza hawajaridhishwa na inabidi wakae wenyewe kujadili hili tuje majibu lakini Baraza linashidwa kuelewa NEMC ni Taasisi ya Serikali ambayo ipo chini ya ofisi ya Makamu wa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kazi yake kubwa ni Kuhakikisha Uifadhi na usimamizi wa Mazingira Kwa Faida ya Taifa Letu .

Baraza hilo maalum ambalo waliwaomba NEMC kuja kutoa Elimu juu ya tathimini ya Athari ya Uhifadhi wa Mazingira katika Mgodi wa bauxite uliopo kata ya Magamba wilaya ya Lushoto ambao waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliomba kusifanyike shughuli zozote za uchimbaji mpaka ije Taasisi ambayo inashughulika na kufanya tathimini ya athari za mazingira katika mgodi huo na kujiridhisha.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Alioneka kutolizishwa na Elimu hiyo na kuwataka NEMC kwenda kutoa vifungu vya Sheria ambavyo vinasema mwekezaji ndiye achague kampuni ya kufanya tathimini ya Athari za Mazingira na Siyo serikali yenyewe bila ya kuelewa Kuwa serikali ndiyo inatoa vibali kwenye hizo Taasisi ambazo zimesajiliwa ili kufanya kazi Kwa ukaribu na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)

Baada ya Baraza hilo kuhitimishwa Mwenyekiti wa Kijiji Cha Magamba Mahamudu Kikoti alisema Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto anaiongopea Serikali kwamba vikao avikufanyika ni jambo la kusikitisha sana Kwa kiongozi Ambaye Sisi kama wasaidizi wake kutoa Taarifa ambazo siyo sahihi na kuhusu Mradi huo na yeye alikuwepo kwenye hivyo vikao vyote Cha Ward Development Meeting WDC Mhtasari wote upo na nimeshauwasilisha Kwa mkuu wa Mkoa Tanga Kwa mikono yangu yote na hizo Taarifa zipo

“Kwa hili nashangaa kuwaambia Nemc awape Taarifa za mhtasari wa Serikali ya Kijiji Wakati hizo Taarifa zipo na yeye anajua hivyo lengo lake kubwa kutaka kukwamisha Mradi usiendelee na kuwapandikiza watu Kuwa Mradi huu una Athari kubwa hivyo wasikubali”

“Alisema mwenyekiti wa Kijiji Cha Magamba Mahamudu Kikoti”.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!