Na Shomari Binda-Musoma
WANANCHI wa Kijiji cha Muhoji Kata ya Bugwema Misoma vijijini wameishukuru serikali kufikiwa na mradi wa maji wa uchimbaji wa visima virefu.
Shukurani hizo wamezitoa mara agosti 26 kijijini hapo mara baada ya mkuu wa Wilaya ya Musoma Dk.Khalfan Haule kupokea gari la uchimbaji visima lililotolewa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Wakizungumza kijijini hapo wananchi hao wamesema kisima kinachochimbwa kwenye Kijiji chao kitawaondoa kwenye adha ya maji waliyokuwa nayo
Wamesema kutokana na kuwa mbali na ziwa victoria wamekuwa wakipata shida ya maji kwa kuyatafuta umbali mrefu rakini Rais Samia amewatua ndoo kichwani
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Happy Mnunguli amesema maji ni huduma muhimu na kutoa shukurani kwa serikali kuwakumbuka.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Musoma mhandisi Edward Sironga amesema kisima kwenye Kijiji hicho kitahudumia zaidi ya watu 4000.
Amesema kwenye Kata hiyo ya Bugwema vitachimbwa visima 4 kati ya 5 vitakavyochimbwa jimbo la Musoma vijijini.
Mkuu wa wilaya ya Musoma Dk Khalfan Haule mara baada ya kupokea gari hilo la mtambo wa kuchimba visima ameishukuru serikali kwa kuwafikia wananchi na kuwapa huduma ya maji
Amesema visima vinachimbwa kwenye changamoto ya vyanzo vya maji na itawasaidia wananchi na kuondokana na shida ya maji.