Home Kitaifa TMA YATOA UTABIRI MWELEKEO WA MVUA ZA MSIMU WA VULI MWEZI OCTOBA...

TMA YATOA UTABIRI MWELEKEO WA MVUA ZA MSIMU WA VULI MWEZI OCTOBA HADI DISEMBA,2024

Na Magrethy Katengu—-Dar es salaam

Mamlaka ya hali ya hewa TMA imesema kuanzia Octoba hadi Desemba 2024 Mvua za chini ya wastani wa katika maeneo mengi zinatarajiwa kuanza kunyesha kwa mtawanyiko na kusuasua huku vipindi virefu vya ukavu katika ardhi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijin Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Dkt. Ladislaus Chang’a amesema mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2024 katika ukanda wa ziwa Victoria na kusambaa katika maeneo mengine katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Octoba, 2024. Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi Disemba ,2024.

Amesema msimu wa mvua za vuli mahususi itakuwa maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki ambapo ni mikoa ya Arusha, Manyara, na Kilimanjaro, Pwani ya kaskazini, kaskazini ya mkoa wa Morogoro, Mikoa ya Pwani (ikijumuisha visiwa vya mafia), Dar es salaam, Tanga na Mikoa ya ukanda wa ziwa Victoria.

Aidha ameelezea Kanda ya Ziwa Victoria mvua za mvuli zinatarajiwa kuwa wastani Hadi chini ya wastani katika mengi ambapo zitaanza wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2024 katika Mikoa ya Geita, Kagera, na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma na kutawanyika maeneo mengine katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Octoba, 2024. Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Disemba , 2024.

Pia amefafanua kuwepo na mvua ya vuli za wastani maeneo ya Pwani , morogoro, visiwa vya mafia , Dar es salaam, Tanga na visiwa vya unguja na Pemba zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya Tatu ya mwezi Oktoba , 2024 na kuisha wiki ya nne ya mwezi Disemba, 2024.

Na nyanda za juu kaskazini Mashariki ambayo ni Mikoa ya Arusha, Manyara, na Kilimanjaro kutakuwa na mvua za wastani hadi wastani kuanza wiki ya tatu ya mwezi Oktoba, 2024 na kuisha wiki ya nne ya mwezi Disemba, 2024.

TMA imesema msimu huo utaathiri shughuli za kilimo ambapo kutakuwa na upungufu wa unyevunyevu kwenye udongo ,kupungua kwa kina cha maji katika mito na mabwawa .

Pia kutakuwa na athari za kiafya ikiwemo kujitokeza magonjwa ya mlipuko kutokana na upungufu wa maji safi na salama .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!