Home Kitaifa MAELFU WAJITOKEZA MAZIKO YA SHEIKH WA WILAYA YA MUSOMA SELEMANI MUSA MAGOTI

MAELFU WAJITOKEZA MAZIKO YA SHEIKH WA WILAYA YA MUSOMA SELEMANI MUSA MAGOTI

Na Shomari Binda-Musoma

MAELFU ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali wamejitokeza kwenye maziko ya Shekh wa Wilaya ya Musoma Selemani Musa Magoti.

Miongoni mwa waliojitokeza kwenye maziko hayo ni Shekh wa mkoa wa Simiyu Issa Kwezi ambaye amemtaja Shekh Selemani kama mmoja wa viongozi wa dini aliyekuwa akihamasisha suala la upendo na amani.

Amesema katika dunia upendo ni suala la muhimu katika dunia ya leo na panapokuwepo na upendo mambo mengine hufanyika.

Amesema katika hotuba ambazo amekuwa akisimama na kuzitoa Shekh Selemani kabla hajafikwa na mauti amekuwa akiumiza kupendana baina ya waumini na jamii kwa ujumla.

Kiongozi huyo wa dini amesema mauti yatosha kuwa waadh kwa wale waliobaki katika kujikita katika kufanya ibada ili kutanguliza mema mbele ya Mwenyezi Mungu.

“Mauti ni waadh unaoelezeka na kila mmoja anapaswa kuushika na kuendelea kufanya ibada kwaajili ya kesho yetu.

” Leo ametangulia Shekh Selemani Magoti baadae zamu yangu na yako kwa hiyo tujiandae kwa kufanya ibada na kutenda yaliyo mema”,amesema Shekh Kwezi.

Shekh wa mkoa wa Mara Msabaha Kassim amesema moja ya mashekh ambao wamekuwa wakimsaidia masuala ya dini ni Shekh Selemani Magoti.

Amesema kila mmoja anatakiwa kuwa mwema kwenye dunia na kubwa ni kuendelea kufanya ibada na kubwa ni kuwa karibu na Mwenyezi Mungu.

Akitoa salamu za serikali Katibu Tawala wa Wilaya ya Musoma Ally Seif Mwendo amesema Shekh Selemani Magoti alikuwa kiunganishi baina ya serikali na viongozi wa dini katika masuala ya kijamii.

Kwa upande wao familia ya marehemu Shekh Suleimani Magoti wamewashukuru wale wote walioshiriki kwenye msiba wa ndugu yao na Shekh wa Wilaya ya Musoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!