Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Mhe. Daktari Selemani Said Jafo amewasihi wataalamu wa afya kuboresha utoaji huduma za afya kwa wananchi.
Dkt. Jafo ametoa rai hiyo wakati akizindua zahanati ya Kijiji cha Chakenge kata ya Mzenge Wilayani Kisarawe. Amesema faraja yake kama kiongozi mwakilishi wa wananchi ni kuona wataalamu hao wanatumia miundombinu ya Afya zilizoboresha Wilayani humo kuanzia ngazi ya Zahanati, Vituo vya Afya Pamoja na Hospitali kutoa huduma iliyobora kwa wananchi.
Dkt. Jafo ameongeza kwamba Ujenzi wa Zahanati hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Malengo waliyojiwekea kama Wilaya kuhakikisha zahanati inazjengwa kila kijiji na Kituo cha Afya kila Kata.
Aidha Dkt. Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe kupelekea vifaa tiba vya kutosha katika Zahanati ya kijiji cha Chakenge ili wananchi waweze kunufaika na huduma za afya karibu na kupunguza safari zisizokuwa za lazima kwenda Kituo cha Afya cha Mzenga.
Pia, amewataka Meneja wa TANESCO na RUWASA Wilayani humo kuhakikisha wanapeleka huduma ya Umeme na Maji katika Zahanati hilo ili kufanikisha upatikanaji wa huduma bila kikwazo