Home Kitaifa ASKARI KATA YA KISANGURA AMSHUKURU MGANGA MFAWIDHI HOSPITALI YA SERENGETI KUSAIDIA JAMII

ASKARI KATA YA KISANGURA AMSHUKURU MGANGA MFAWIDHI HOSPITALI YA SERENGETI KUSAIDIA JAMII

Na Shomari Binda-Serengeti

ASKARI poiisi Kata wa Kata ya Kisangura iliyopo wilayani Serengeti mkoani Mara Genuine Kimario amemshukuru mganga mfawidhi wa hospital ya wilaya hiyo Joseph Muhere kuguswa na kusaidia jamii.

Shukrani hizo zimepelekwa pia kwa mganga mkuu wa wilaya ya Serengeti Dk.Adam Lusubilo kwa pamoja kufanikisha kupatikana kwa baiskel mbili za magurudumu matatu ( Will Chair) kusaidia wenye ulemavu.

Akizungumza na Mzawa Blog jana Agosti 16,2024 askari Kata huyo amesema moja ya majukumu yake ni kuifikia jamii na kujua changamoto na kuweza kusaidia.

Amesema askari hana kazi ya kukamata pekee bali jamii inazo changamoto nyingine ambazo hata askari wa jeshi la polisi analo jukumu la kushirikiana kupata ufumbuzi.

Askari huyo mwenye cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi akiwa askari Kata wa Kata ya Kisangura amesema katika majukumu yake ya kazi alizitembelea jamii zenye watu wanaoishi na ulemavu wanaohitaji msaada na kufanya jitihada za kuwasaidia.

Amesema jamii za familia mbili alikutana nazo kwenye Kitongoji cha Kibakonga zikiitaji msaada wa baiskel kwaajili ya kutembelea na kutafuta wadau wa kuweza kusaidia.

” Nishukuru ofisi ya ustawi na maendeleo ya jamii kwa kufanikisha kukutana na mganga mdawidhi wa hospital ya wilaya ya Serengeti Dk.Muhere na mganga mkuu wa Wilaya kwa juhudi zao kupata baiskel hizi.

” Madaktari hawa wameguswa na wenyewe wanajua namna zilivyipatikana na kusaidia jamii hii ambayo ilikuwa na uhitaji tunawashukuru sana”,amesema.

Askari huyo amezitaja familia zilizosaidiwa msaada huo kuwa ni mzee Benjamin Imori aliyepooza upande mmoja na mtoto Wakuru Ntagirama ambaye alizaliwa na ulemavu.

Familia zilizopata msaada zimemshukuru askari Kata huyo kwa kuwatembelea na kuguswa na kusaidia kufanikisha kupatikana kwa baiskel hizo.

Aidha familia hizo zimeiombaam jamii kuguswa na wenye uhitaji na kujitoa kusaidia kupata msaada.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!