Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Mhe. Dkt Selemani Jafo ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara ameisitiza Wakala wa Maji Usafi wa Mazingira Vijiji (RUWASA) Wilayani Kisarawe kuweka mazingira rafiki kwa wananchi wanaotaka kuvuta maji majumbani mwao.
Dkt. Jafo ametoa rai hiyo akizungumza mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Mtu nani Kata ya Vikumburu wilayani humo akiwa katika ziara ya kuwasilisha utekelezaji wa ilani jimboni pamoja ma kusikiliza na kutatua kero za wwananchi.
Amesema hatua hiyo itawawezesha wananchi kulipa gharama halisi ya maji waliyotumia na kupunguza manung’uniko miongoni mwa wananchi.
Aidha Dkt. Jafo amewasihi wananchi kulinda moundombinu ya miradi hiyo ili iweze kudumu na kumaliza kabisa shida ya upatikanaji wa maji salama na salama karibu na jamii kama ilivyodhamira ya serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kumtua mama ndoo Kichwani.